Kaya 21 Bunda zaiangukia serikali kulipwa fidia

Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Kyandege wilaya ya Bunda mkoani Mara wakionyesha nyumba zilizobomolewa kijijini hapo  kwaajili ya kupisha mradi wa ujenzi wa barabara ya Sanzate - Natta na kudai ubomoaji huo haukufanyika kwa haki kwani wanazo sifa za kulipwa fidia. Picha na Beldina Nyakeke

Muktasari:

Kaya 21 katika kijiji cha Kyandege wilayani Bunda mkoa wa Mara zimeiomba serikali kuangalia namna ambavyo itawasaidia bada ya nyumba zao kubomolewa kwaajili ya kupisha mradi wa ujenzi wa barabara ya Sanzate - Natta yenye urefu wa kilomita 40.

Bunda. Kaya 21 katika kijiji cha Kyandege wilayani Bunda mkoa wa Mara zimeiomba serikali kuwawasaidia baada ya nyumba zao kubomolewa kwa ajili ya kupisha mradi wa ujenzi wa barabara ya Sanzate - Natta yenye urefu wa kilomita 40.


Wakizungumza kijijini hapo leo Novemba 8,2022 wakazi hao wamesema kuwa wameshtushwa na uamuzi wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroads) mkoa wa Mara wa kuwataka kupisha katika maeneo yao bila kulipwa fidia  wakati wanaamini maeneo  hayo ni ya yao kihalali.


“Mimi nimeishi hapa tangu mwaka 1974 kipindi cha operesheni kijiji na hii barabara haikuwepo isipokuwa ilikuwepo njia ya kupitisha ng'ombe kwenda mnada wa Mugeta lakini leo natakiwa kupisha bila kulipwa fidia,” amesema Philipo Ngea.


Ngea amesema kuwa kutokana na nyumba zao kuvunjwa hivi sasa hawana mahali pa kuishi hivyo kuiomba serikali kuangalia namna ambavyo itawasaidia ili waweze kuendelea na maisha kama ilivyokuwa awali.


Mkazi mwingine Joseph Kasanda amesema baada ya kutakiwa kubomoa nyumba zao waliamua kwenda mahakamani kudai haki zao ambapo mahakama iliamuru  wamiliki wa nyumba sita kati ya 21 zilizotakiwa kubomolewa kulipwa fidia kwa mujibu sneria na tarayubu maamjzi amhayo hata hivyo hayakutekelezwa.


“Tunashangaa hizi nyumba sita ambazo pia mahakama iliamuru zilipwe fidia nazo zimebomelewa bila u fidia hii inaonyesha kuna kitu hakiko sawa tunaiomba serikali iingilie kati sote kwa umoja wetu tulipwe tupishe mradi uendelee,” amesema Kasanda.


Mkazi mwingine, Samson Kasanda amesema kuwa wanashangaa kuona barabara hiyo kuongezewa upana wakati ni barabara ya wilaya ambayo kisheria inatakiwa kuwa na mita 10 pekee na kwamba utaratibu wa kupandisha hadhi barabara hiyo hadi kuwa ya mkoa haukuwahi kufanyika.


Amesema kuwa kutokana na nyumba za kubimloewa hivi sasa wa.eoata hifadhi kwa ndugu zao jambo ambalo sio zuri hivyo kuimba kuwezeshwa ilinwawese kujenga nyumba za kuishi.


Akizungumzia madai hayo, Meneja wa Tanroads mkoa wa Mara, Vedastus Maribe amesema barabara hiyo ni moja ya barabara kuu zinazosimamiwa na ofisi yake mkoani humo.


Amesema kuwa kabla ya kuanza utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara tathmini ilifanyika ambapo watu wote wenye sifa za kulipwa fidia walilipwa na kwamba wanaolalamika hawana sifa kwa mujibu wa  sheria.


“Hii barabara inajengwa kwa thamani ya Sh39 bilioni na kwa suala la fidia tumelipa zaidi ya Sh700 milioni kwa eneo lote la mradi kikiwemo kijiji cha Kyandege, kwa hiyo hakuna mtu ambaye ameonewa,” amesema.


Amesema kaya hizo katika kijiji cha Kyandege zilikwenda mahakamani kudai kudhulumiwa haki zao ambapo mahakama iliamuru nyumba sita kati ya 21 kulipwa fidia lakini serikali ilikata rufaa dhidi ya maamuzi hayo ambapo wahusika hao walishindwa kuthibitisha mahakamani juu ya uhalali wao, hivyo wote kutakiwa kupisha mradi uendelee kwani walikuwa wamevamia eneo la hifadhi ya barabara.