Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

KCBL yatakiwa kuwa na sura ya kitaifa

Mtendaji Mkuu wa benki ya ushirika ya Kilimanjaro (KCBL), Godfrey Ng'ura akizungumza wakati wa hafla ya kutoa taarifa ya mwaka mmoja wa benki hiyo. Picha na Janeth Joseph

Muktasari:

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Andrew Massawe ameutaka uongozi wa Benki ya Ushirika ya Kilimanjaro (KCBL) kuharakisha mchakato wa benki hiyo kuwa  benki yaUshirika ya  kitaifa.

Moshi. Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Andrew Massawe ameutaka uongozi wa Benki ya Ushirika ya Kilimanjaro (KCBL) kuharakisha mchakato wa benki hiyo kuwa  benki yaUshirika ya  kitaifa, hatua mbayo itakuwa chachu ya maendeleo nchini hususani sekta ya kilimo na ushirika.

Amesema kukamilika kwa mchakato huo wa kuwa benki ya ushirika ya Kitaifa itakuwa ni mkombozi mkubwa kwa wakulima nchini pamoja na vyama vyote vya Ushirika.

Ameyasema hayo leo wakati wa hafla fupi  ya kutoa taarifa ya mwaka mmoja wa mafanikio ya benki hiyo ambapo amesema katika kipindi cha mwaka jana, benki hiyo imepata faida kabla ya kodi ya Sh54 milioni  ikilinganishwa na hasara ya milioni 600 iliyopata mwaka 2020.

"Nitoe wito Mrajisi wa vyama vya ushirika, Dk Ndiege, ikiwezekana ubaki Moshi uhamishie ofisi hapa kukamilisha suala la kuifanya KCBL kuwa benki ya kitaifa ya ushirika, baada ya hapo ndio uje nayo Dodoma ambako ni makao makuu ya nchi," amesema

Pamoja na mambo mengine ameiiomba benki ya CRDB kuendelee kuisaidia benki hiyo ya Ushirika  ili iweze kufikia mtaji wa 15 bilioni na kukidhi vigezo vya kuwa benki ya taifa ya ushirika.


"CRDB tunaomba muendelee kuisaidia benki hii ili iweze kufikia mtaji wa Sh15 bilioni na serikali imedhamiria kuendelea kuisaidia ili kufanikisha malengo ya kuiwezesha kuwa benki ya Taifa ya ushirika ifikapo mwezi ujao"amesema Massawe

"Tume ya maendeleo ya ushirika nchini chini ya mrajisi iendelee  kuisimamia benki hii ya ushirika, imetokea kwenye hali ngumu sana, changamoto nyingi lakini sasa tukaisimamie lwa kufuata miongozo, sheria, kanuni na taratibu zilizopo na wizara tutahakikisha tunaendelea kuboresha sera na sheria za ushirika nchini"

Katika hatua nyingine Massawe ametoa wito kwa Vyama vya Ushirika kote nchini kuwekeza na kununua hisa za KCBL kama ilivyoelekezwa  na Waziri wa Kilimo katika mkutano mkuu wa vyama vya Ushirika (TFC) Desemba mwaka jana 2021 ikiwa ni pamoja na Vyama vyote vya mazao kutenga kiasi cha fedha ili kununua hisa na kukidhi takwa la kimtaji la kuwa na Benki ya Taifa ya Ushirika.

“Vilevile vyama vya fedha vya Akiba na Mikopo (SACCOS) pia vitoe fedha kupitia matengo maalum ya kibajeti kwa mwaka 2022. Nitoe rai pia kwa Wafanyabiashara, taasisi za umma na binafsi, watu binafsi na wadau wote wa maendeleo kuunga juhudi zetu za kuwa na Benki ya Taifa ya Ushirika” Aliongeza Massawe.

Naye Mtendaji Mkuu wa Benki ya Ushirika Kilimanjaro (KCBL) Godfrey Ng’urah amebainisha mikakati ya Benki hiyo ni pamoja na kukuza mtaji hadi kufikia Sh20 bilioni ikiwa ni mkakati wa muda mfupi na sh 50 bilioni ndani ya miaka mitano (5) ijayo.

Amesema, mafanikio hayo yanakuja ikiwa ni mwaka mmoja wa jitihada za Serikali kwa Kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) pamoja na Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini kuinurusu Benki ya Ushirika ya Kilimanjaro (KCBL) ambapo kupitia jitihada hizo Benki ya CRDB iliwekeza kiasi cha sh7bilioni pamoja na kutoa msaada wa usimamizi kwenye Menejimenti na Bodi ili kuimarisha usimamizi na weledi kwa kwa miaka 3.

Amesema ukuaji wa mtaji pamoja na amana mpaka sasa benki hiyo  ina jumla ya amana za wateja za Sh 5.5 bilioni pamoja na ongezeko la fedha za wanahisa kutoka Sh1.8 bilioni hadi Sh 2.9 bilioni.

"KCBL tumeendelea kuingiza sokoni huduma na bidhaa bunifu  ikiwemo huduma za kadi zenye chapa ya kimataifa ya KCBL, VISA CARD, huduma za ATM, pamoja na KCBL Wakala."amesema Ng'urah