Kenya yasogeza mbele siku za kufungua shule

Muktasari:

  •  Waziri wa Elimu nchini, Kenya George Magoha leo Jumamosi, Agosti 13, 2022 ametangaza kusogeza mbele tarehe ya kufungua shule za Taasisi za elimu ya msingi kutoka Agosti 15 kama alivyotangaza awali hadi Agosti 18.


Nairobi. Waziri wa Elimu nchini, Kenya George Magoha leo Jumamosi, Agosti 13, 2022 ametangaza kusogeza mbele tarehe ya kufungua shule za Taasisi za elimu ya msingi kutoka Agosti 15 kama alivyotangaza awali hadi Agosti 18.

Hii ni mara ya pili kwa Kenya kusogeza mbele kufunguliwa kwa shule kwa kuwa mwanzoni walitangaza kufungua Agosti 11, 2022 lakini kutokana na zoezi la kuhesabu kura kutokamilika mapema wakasogeza hadi Agosti 15, 2022.

Hata hivyo kabla Agosti 10 waziri huyo alijitokeza tena mbele ya vyombo vya habari na kuisogeza mbele tarehe hyo hadi kufika Agosti 15,2022 ambayo pia leo ameisogeza hadi Agosti 18, 2022 ambapo inatarajia pia kura za urais zitakuwa tayari zimetangazwa.

“Kufuatia mwenendo wa Uchaguzi wetu wa uliofanyika jumanne Agosti 9, 2022 mchakato wa kujumlisha kura bado unaendelea. Kwa hiyo, kufuatia mashauriano zaidi, nawasilisha uamuzi wa Serikali kuhusu kusimamisha ufunguaji upya wa shuleza Taasisi zote za elimu ya Msingi ambao ulitakiwa kufanyika Agosti 15, 2022 hadi Alhamisi, Agosti 18, 2022,” amesema

"Taarifa hii inachukua nafasi ya taarifa zote za awali zilizowahi kutyolewa kuhusu ufunguaji wa Taasisi zote za elimu ya msingi nchini,” aliongeza.