Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kesi ya Kipande yakwama baada ya hakimu kuhamishwa

Muktasari:

  • Kesi Inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari ya Tanzania (TPA), Madeni Kipande na wenzake wanne imeshindwa kuendelea baada ya Hakimu Mkazi Mkuu, Ramadhani Rugemalira anayeendesha shauri hilo kuhamishwa.

Dar es Salaam. Kesi Inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari ya Tanzania (TPA), Madeni Kipande na wenzake wanne imeshindwa kuendelea baada ya Hakimu Mkazi Mkuu, Ramadhan Rugemarila anayeendesha shauri hilo kuhamishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Madeni na washtakiwa wenzake wanne wanakabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh4.2 bilioni.

Wakili wa Serikali, Grory Kilawe alidai hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,  Mary Mrio kuwa hakimu aliyekuwa anaendesha shauri hilo amehamishwa hivyo aliiomba mahakama hiyo ipange tarehe nyingine ya kutajwa.

"Hakimu amehamishwa hivyo naiomba mahakama hii apangiwe tarehe nyingine ya kutajwa ili wasubili kupangiwa hakimu mwingine," alidai Kiwale.

Hakimu Mrio aliahirisha shauri hilo hadi Agosti 31, 2023 kwa ajili ya kutajwa huku washtakiwa hao wapo nje kwa dhamana.


Mbali na Kipande washtakiwa wengine wengine  ni Peter Gawile (58) Ofisa Rasilimali Watu wa TPA, Casmily Lujegi (65)  Mwenyekiti wa Bodi  ya Manunuzi wa TPA, Mashaka Kisanta (59) Mkurugenzi Idara ya Manunuzi na Kilian Chale (51) Kaimu Mkurugenzi Idara ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na mkazi wa Mbezi Makabe.

Inadaiwa kati ya Oktoba Mosi,2014 na Oktoba Mosi 2020 jijini  Dar es Salaam, walikula njama na kuisababishiaTPA hasara ya Sh4.2 bilioni.

Inadaiwa washtakiwa hao walitangaza zabuni hiyo, bila kupata kibali cha Bodi ya Zabuni mamlaka hiyo na kushindwa kufuata kanuni za zabuni hivyo kutoa malipo ya awali ya asilimia 40 bila idhini ya bodi hiyo jambo lililosababisha TPA hasara ya Dola za Marekani milioni 1.8 sawa na zaidi ya Sh4.2 bilioni.