Kesi ya uhaini 1982: Baba, mwana wafichua matumizi ya ndege sita za wanamaji kortini -7

Kesi ya uhaini 1982: Baba, mwana wafichua matumizi ya ndege sita za wanamaji kortini -7

Muktasari:

  • Jumatano Januari 23, 1985, baba na mwanawe walitoa ushahidi upande wa mashtaka katika kesi ya uhaini ambayo mmojawao alisema ndege sita za Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) zingetumika kuwatisha na kuwavuruga wananchi siku tatu baada ya Serikali ya Mwalimu Julius Nyerere kuangushwa.

Jumatano Januari 23, 1985, baba na mwanawe walitoa ushahidi upande wa mashtaka katika kesi ya uhaini ambayo mmojawao alisema ndege sita za Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) zingetumika kuwatisha na kuwavuruga wananchi siku tatu baada ya Serikali ya Mwalimu Julius Nyerere kuangushwa.

Akitoa ushahidi wake kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania mjini Dar es Salaam iliyosikiliza kesi hiyo iliyowakabili Watanzania 19 wakiwamo wanajeshi 14, Luteni Augustine Pancras Ndejembi, ambaye ni mtoto wa Pancras Ndejembi aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma wakati kesi hiyo ikiwa mahakamani, alisema kikosi cha Jeshi cha Wanamaji pia, kingetumiwa kufanya kazi hiyo ya kuwatisha na kuwavuruga wananchi.

Habari kamili bonyeza hapa https://egazeti.co.tz/show_related/8514