Kikwete, Hichilema wamlilia Askofu Mwanisongole

Muktasari:
Rais Mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete na Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema ni miongoni mwa viongozi wa waliotuma salaam za pole kwenye mazishi ya Askofu Mkuu Mstaafu wa Tanzania Assembles of God (TAG), Dk Ranwell Mwanisongole.
Songwe: Rais Mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete na Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema ni miongoni mwa viongozi wa waliotuma salaam za pole kwenye mazishi ya Askofu Mkuu Mstaafu wa Tanzania Assembles of God (TAG), Dk Ranwell Mwanisongole.
Ibada ya kumuaga Askofu Mwanisongole alifariki dunia Jumamosi Desemba 25, 2021 katika hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam imefanyika leo Alhamisi Desemba 30, 2021 katika uwanja wa CCM Vwawa mkoani Songwe.
Akizungumza kweneye ibada hiyo, Askofu Mkuu wa TAG, Barnabas Mtokambali amewashukuru viongozi wakuu akiwataja kuwa ni pamoja na Rais Samia Suluhu Hassan , Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema na Rais Mstaafu wa awamu ya nne nchini, Jakaya Kikwete kwa salaam zao za faraja.
Aidha amewashukuru Viongozi wengine na watu mbalimbali waliofika kwenye mazishi hayo mkoani Songwe.
Marehemu Askofu Ranwell Mwenisongole anazikwa katika makaburi ya familia yaliyopo katika maeneo ya Ichenjezya katika mamlaka ya mji wa Vwawa.