Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kilichowaponza wafanyabiashara kufungiwa maduka

Baadhi ya maduka yaliyopo eneo la nunge Manispaa ya Morogoro ambayo yamefungwa baada ya wamiliki wake kukiuka masharti ya biashara. Picha Hamida Shariff

Muktasari:

  • Wafanyabiashara wa bidhaa za jumla eneo la Nunge Manispaa ya Morogoro wameonywa tabia ya kuhifadhi vibaya bidhaa za maji, vyakula na juisi ikitajwa baadhi ya bidhaa zinaathirika ubora baada ya kupigwa na vumbi, kunyeshewa mvua na jua.

Morogoro. Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro imelazimika kuyafunga baadhi ya maduka yaliyopo katikati ya mji huo baada ya wamiliki wake kuendelea kupanga bidhaa zao nje ya maduka hayo licha ya kupewa onyo mara kadhaa.

Pamoja na kuyafunga maduka hayo lakini pia wamiliki wametakiwa kulipa faini ya Sh500,000 hali iliyowafanya kwenda ofisini kwa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Rebeca Nsemwa wakishinikizwa kufunguliwa maduka yao.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Jumatano Oktoba 25, 2023 mjini hapa, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, Ally Machela amesema Manispaa ya Morogoro imechukua hatua hiyo baada ya baadhi ya wafanyabiashara kukiuka masharti ya biashara.

Machela amesema sababu iliyopelekea Manispaa kuwatoza faini baadhi ya wafanyashara imetokana na sababu ya kuweka bidhaa za maji, juisi na vyakula kinyume na sheria lakini eneo la nje kukeuza kuwa stoo za biashara zao na kupekea adha kwa vyombo vya moto na watumiaji wa barabara.

“Baadhi ya wafanyabiashara wametozwa faini ya Sh500,000 badala ya Sh1 milioni kwa kosa la kuweka bidhaa nje ya duka na kugeuza eneo la duka kuwa stoo ya kuhifadhia bidhaa zao na baadhi ya biashara haziruhusiwi kunyeshewa na mvua, jua, vumbi ili kulinda viwango vya bidhaa husika lakini bidhaa hizo zimekuwa zikihifadhiwa ndani ya hifadhi ya barabara na kusababisha kero kwa watumiaji,”amesema Machela.

Katibu wa Wafanyabiashara Mkoa wa Morogoro, Hussein Chalela amesema kabla ya maofisa biashara kuendesha shughuli yoyote zifanyike juhudi za kukutanisha wafanyabiashara ili kuepusha adha inayoweza kujitokeza na kumuathiri mfanyabiashara na biashara yake.

“Wafanyabiashara 15 wamepigwa faini kwa kosa la kuweka bidhaa nje ya duka lakini kujenga sehemu ya kuhifadhia bidhaa kinyume na taratibu na tunamshukuru DC Rebeca Nsemwa kwa kuzuia zoezi hili ambalo wafanyabiashara zaidi ya 40 wa bidhaa za jumla eneo la Nunge wangekutana na rungu la kupigwa faini na sasa ametoa siku saba wafanyabiashara wote waliokiuka warekebishe kasoro hizo,”amesema Chalela.

Akizungumza na wafanyabiashara waliokusanyika ofisini kwake kulalamika juu ya kupigwa faini hizo, Mkuu wa Wilaya ya Morogoro hiyo, Rebeca Nsemwa amesema tayari ametoa maagizo kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro kusitisha zoezi la kuwapiga faini wafanyabiashara wote waliokiuka taratibu za leseni za biashara.

“Nimetoa siku saba kwa ofisi ya Mkurugenzi kusitisha zoezi la kuwapiga faini wafanyabiashara wote waliokuwa katika orodha ya kutozwa faini na badala yake kila mfanyabiashara arekebishe eneo lake la duka kwa ndani ya siku saba waondoe bidhaa zote na kubomoa stoo zilizojengwa eneo la duka na tutaonyesha mfano nzuri wa kuweka bidhaa nje bila kuathiri biashara na watumiaji wa barabara,”amesema.

Nsemwa amesema kuwa aliwataka wakaguzi wa maduka pamoja na TRA kujitambulisha kwa kuonesha vitambulisho kwa wafanyabishara wanaokwenda kuwakagua ili kuepuka matapeli ambao wamekuwa wakiwatisha kuwa wao ni wakaguzi na hivyo kuwatoza faini zilizoeleweka.