Kilimo cha kuhamahama chahatarisha Hifadhi Msitu wa Rondo

Mzee Christopher Magnus mkazi wa Rondo akifanya usafi katika shamba la miti la Msitu wa Hifadhi ya Rondo iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtama Mkoani Lindi. Picha na Florence Sanawa

Muktasari:

  • Kilimo cha kuhamahama kimetajwa kuhatarisha Hifadhi ya Msitu Rondo hali ambayo huwalazimu kuweka vitu vya kukinga moto kuzunguka mashamba yote kila inapofika mwezi wa 6 na 7 kuzuia moto usiingie katika hifadhi.

Lindi.  Wananchi wanaoshi katika vijiji vilivyopo pembezoni mwa Hifadhi ya Msitu Rondo wametakiwa kuacha ulimaji wakuhamahama ili kuweza kuepuka moto unaoweza kuharibu mazingira ya Hifadhi ya Msitu wa Rondo iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtama mkoani Lindi.

Akizungumza na waandishi wa habari wa mikoa ya Lindi na Mtwara waliotembelea hifadhi hiyo Muhifadhi Mkuu Rondo Samson Mweta alisema kuwa msitu huo unasimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na una ukubwa hekta 2979.1 hivyo kuwa na kazi kubwa ya kudhibiti moto kuingia katika hifadhi hiyo.

“Unajua vyanzo vya majanga ya moto ni kilimo wakati wa kuandaa mashamba kilimo cha kuhamahama chanzo kikubwa cha wakati wanaandaa mashamba moto huwaponyoka na kuingia kwenye hifadhi,”amesema.

“Tukizalisha miche tunaipanda shambani ambapo hupaliliwa na kuifyekea kisha kufanya upunguziaji wa matawi kwakusafisa kulinda msitu dhidi ya moto ambapo huwa tunafyekea kwa kutengeneza barabara ili kuzuia moto kinga moto kuanzia mwezi wa 7,8 na 9,” amefafanua.

“Hali ya hewa imeimarika ni mara nyingi mvua huanzia hapa na kuishia hapa chanzo cha maji cha mito mingi ambapo viunga 67 ambavyo vimepandwa miti aina mbalimbali kama vile msindano, mikaratusi mitiki mipira na miti mingine mingi,” amesema Mweta.

Naye Christopha Magnus mkazi wa Rondo alisema kuwa mbali na kupewa miche ya miti pia wamekuwa wakipata elimu namna gani sahihi ya kutunza maizngira ya hifadhi hiyo.

“sisi ni wakazi wa hapa tunapata ajira ndogo ndogo katika msitu huu na tunapambana kuhifadhi mazingira, tumekuwa tukipwewa miche ya miti bure ambayo tunapata katika mashamba yetu. Mpaka sasa tumefanikiwa kuhamasisha tuna zaidi ya miaka mitano moto haujauinga ndani ya hifadhi,” amesema.

Katibu wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mtwara, Bryson Mshana amesema kuwa utolewaji wa elimu kwa wananchi wanaozunguka hifadhi kutasidia kuokoa mazingira.

“ziara imekuwa ya mafanikio makubwa kwa wanahabari tumefahamu juu ya kuotesha mbegu na utunzaji ya misitu hifadhi hii ina vitu vingi ambavyo awali watu wengi walikuwa hawavifahamu hata sisi tulikuwa hatufahamu,” amesema.