Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kiwanda cha Chanzi Arusha hatarini kufungwa

Meneja uzalishaji  wa kiwanda cha Chanzi, Mayasa Mhina akizungumza kiwandani  hapo

Muktasari:

  • Harufu kali na mbaya inayotoka katika kiwanda cha Chanzi imekuwa tishio kwa afya za binadamu kutokana na kiwanda hicho kuwa katika makazi ya watu.

Arusha. Baraza la Taifa la Hifadhi za Usimamizi wa Mazingira NEMC limetoa siku saba kwa mmiliki wa  kiwanda cha kuzalisha virutubisho vya mifugo cha Chanzi kilichopo Njiro jijini Arusha, kudhibiti harufu kali na mbaya inayotoka kiwandani hapo na kusababisha athari za kimazingira na afya kwa jamii.

Aidha baada ya muda huo kumalizika bila utekelezaji, NEMC itachukua hatua kali ikiwemo kukipiga faini ama kukifunga kiwanda hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 22, 2023 jijini Arusha mara baada ya kufanya ukaguzi wa kushtukiza katika kiwanda hicho, Kaimu Mkurugenzi wa uzingatiaji na utekelezaji wa sheria NEMC, Dk Thobias Mwesiga amesema ni mara ya pili kwa NEMC kufika kiwandani hapo na kutoa maelekezo ambayo yamekuwa hayatekelezwi .

"Kama tukija tena kwa mara ya tatu tukakuta bado malalamiko ya wananchi wanaozunguka maeneo haya yanaendelea, tutawapiga faini au kukifunga kiwanda kabisa ili waweza kuchukua hatua hadi hapo tutakapojiridha wameondoa tatizo," amesema.

Aidha Dk Mwesiga ameagiza halmashauri ya Jiji la Arusha kukamilisha haraka mchakato wa kukihamisha kiwanda hicho kutoka kwenye makazi ya watu ili kunusuru wananchi wanaoendelea kuathirika na harufu inayotoka kiwandani hapo.

Amesema NEMC imekuwa ikitoa maelekezo kadhaa kwa mmliki wa kiwanda hicho juu ya malalamiko ya wananchi kuhusu harufu kali na kwamba mara ya mwisho walimwandikia barua Mei 23 mwaka huu ya kurekebisha kasoro, lakini ameshindwa kutekeleza na ndio maana wamelazimika kufika tena kiwandani hapo na kutoa onyo la mwisho.

Dk Mwesiga amefafanua kuwa lengo la Baraza sio kufunga kiwanda ila ni kumwelimisha kwanza mzalishaji na baada ya hapo kama bado ameshindwa kuzingatia masharti hatua kali zinachukuliwa dhidi yake.

Naye Ofisa mazingira wa Jiji la Arusha, Sigfrid Mbuya amesema halmashauri ipo katika hatua ya mwisho kukamilisha mchakato wa kumpatia eneo jingine mmiliki wa kiwanda hicho ili aweze kukihamisha katika makazi ya watu.

Amesema kiwanda hicho kimekuwa msaada mkubwa kwa Jiji la Arusha kwa kukusanya taka ngumu takribani tani 25 na kuzigeuza fursa ya ajira kwa kuzalisha virutubisho vya mifugo na biogesi.

Hata hivyo amesema pamoja na nia njema ya kiwanda hicho, athari za kiafya kwa wananchi ni kubwa hivyo halmashauri kupitia vikao vyake inakamilisha mchakato wa kuwapatia eneo hilo ili kukiondoa katika makazi ya watu.

Naye Meneja uzalishaji wa kiwanda cha Chanzi, Mayasa Mhina amesema changamoto ya harufu mbaya na kali inayotoka kiwandani hapo sio ya kila siku ila imesababishwa na kukatika mara kwa mara kwa nishati ya umeme.

Amesema kiwanda hicho kimekuwa kikikusanya takribani tani 25 ya taka ngumu kwenye masoko ya mjini hapa na lengo ni kufikisha tani 65 kwa siku jambo ambalo wanaendelea kuimarisha uzalishaji.

"Wapo mbioni kutumia teknolojia mpya kutoka nchi jirani ya Kenya itakayosaidia kuondoa harufu kali za taka na wataanza kuitumia kwa sasa wakati wakisubiri mchakato kukamilika wa kuhamisha kiwanda hicho," amesema.