Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

NEMC yalia na wanaochimba dawa vichakani

Muktasari:

  • NEMC imelivalia njuga suala la baadhi ya mabasi ya mikoani kuchimba dawa katika mapori na kutangaza kuanza kutoa elimu kwa umma wiki ijayo kabla ya kuchukua hatua kwa watakaobainika.

Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dk Samuel Gwamaka amesema kuanzia wiki ijayo wataanza kutoa elimu kwa umma na wamiliki wa mabasi kuhusu kuzingatia usafi wa mazingira wanapokuwa safari katika mikoa mbalimbali.

Amesema kwa siku za karibuni kumekuwa na tabia ya za baadhi ya mabasi kusimamia porini na kutoa fursa kwa abiria wao kuchimba dawa jambo badala ya kuwapeleka katika vyoo vilijengwa katika halmashauri au vituo vya mafuta.

Dk Gwamaka ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Agosti 31, 2023 wakati akizungumza na wanahabari kuhusu umuhimu wa Watanzania kuzingia usafi wa mazingira katika usafiri wa umma ikiwemo daladala na mabasi ya mikoani.

Amesema katika mchakato huo, NEMC itashirikiana na Mamlaka ya Usafiri wa Ardhini (Latra) na halmashauri mbalimbali nchini, akisema elimu hiyo itatolewa kwa muda wa mwezi mmoja kisha hatua za adhabu zitafuatwa kwa watakaobainika kukiuka utaratibu.

"Kumekuwa na tabia ya mabasi kusimama porini na kuamuru abiria kushuka na kuchimba dawa kwa kuwaga wanawake upande huu na mwanaume upande ule.Hili jambo limekuwa kwa muda mrefu na limeleta kero katika jamii.

"Sio tu kuchafua mazingira bali linadhalilisha wengi tumeona maana maeneo mengine sio rafiki hasa kwa wanawake, pia ni hatarishi maana kuna sehemu zingine ni mapori.Tumeamua kuliweka wazi kwa jamii ili vyoo kujengwa kila baada ya maeneo kadhaa," amesema Dk Gwamaka.

Dk Gwamaka amesema wataelimisha umma kupitia vyombo vya habari na maeneo ya stendi kuu za mabasi yaendayo masafa marefu.Amesema wamedhalimia kuhakikisha wenye mabasi kuchukua wajibu kuelimisha pia wao kabla ya kuanza safari.

Kwa mujibu wa Dk Gwamaka, mchakato wa kutoa elimu ukiisha hatua inayofuata ni kutoa adhabu isiyopungua ya faini ya Sh5 milioni kwa watakaobainika kukiuka utaratibu huo, huku akiwaomba wananchi kutoa ushirikiano wa kupiga picha za mabasi yatakayofanya vitendo hivyo.

"Wewe piga picha itume kwetu, tutatoa motisha kwa atakayefanikisha ingawa hatuwezi kuisema ya aina gani kwa sasa, ila tunaaanza na elimu kwanza ambayo ni muhimu katika hatua hii kabla ya hatujafika huko.

"Kuanzia Oktoba 2 mwaka huu hatutegemei kuona basi lolote likichimba dawa katika eneo lisiloruhusiwa, tunasisitiza wanaonunua mabasi basi wahakikishe yanakuwa na huduma za vyoo ndani," Dk Gwamaka.


Hata hivyo, Dk Gwamaka amewapongeza wamiliki mabasi akisema baadhi yao wamepiga hatua kwa vyombo vyao vya usafiri kuwa na huduma ya choo ndani. Amesema huo ndio mwelekeo sahihi kwa mabasi katika kukabiliana na changamoto hizo kwa sababu wanabeba abiria wa aina tofauti.