Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

KKKT Kusini Mashariki yapata askofu mpya, ibada zarejea

Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT TANZANIA  Fredrick Shoo (aliyevaa kofia ya kijani) pamoja na Katibu Mkuu wa Kanisa hilo Mhandisi Robert Kitundu(wa kwanza kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Askofu Mstaafu wa Dayosisi ya Kusini Mashariki wa Kanisa Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Lucas Mbedule Judah(wanne kushoto) pamoja na Askofu mteule Yeriko Ngwema(wapili kushoto) baada ya kumalizka uchaguzi. Picha na Florence Sanawa

Muktasari:

  • Kanisa la Kiinjili la Kulitheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kusini Mashariki imepata Askofu mpya Mchungaji Yeriko Ngwema Mchungaji Geofrey Mposola akiwa msaidizi wake.

Mtwara. Hatimaye matumaini ya kurejea kwa ibada katika Kanisa la Kiinjili la Kulitheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kusini Mashariki mkoani Mtwara yanaonekana, baada ya kupatikana kwa uongozi mpya wa nyumba hiyo ya ibada ya waumini wa dini ya kikristo.

Kupatikana kwa uongozi mpya, kumetokana na uchaguzi uliofanyika Julai 18, mwaka huu uliomchagua Mchungaji Yeriko Ngwema kuwa askofu mteule wa kanisa hilo, huku Mchungaji Geofrey Mposola akiwa msaidizi wake.

Uchaguzi huo uliotanguliwa na Mkutano wa Sinodi wa Julai 17, 2023, umefanyika miezi minne baada ya kuisha kwa fukuto la migogoro ndani ya kanisa hilo, lililodumu kwa zaidi ya miaka sita.

Mgogoro ndani ya kanisa hilo, uliochagizwa na kutotakiwa kwa Askofu Lucas Mbedule aliyekuwa kiongozi na kwamba umekoma Machi mwaka huu, baada ya Mkuu wa KKKT, Askofu Frederick Shoo kuunda kamati ya watu 11, kuushughulikia.

Akizungumza katika misa maalum baada ya uchaguzi huo, Askofu Shoo ambaye pia alishiriki mkutano wa Sinodi, alimtaka Ngwema kuhakikisha kiti cha uaskofu kinarejea ndani ya kanisa kuu ili ibada ziendelee.

Kwa mujibu wa Askofu Shoo, kwa muda mrefu kiti cha uaskofu hakikuwa ndani ya kanisa hilo hivyo ni vema kikarudishwa.

“Nasisitiza kuwa kuanzia jumapili ijayo hakikisheni kiti cha askofu kinarudi kanisani sameheaneni katika pendo la kristo, naamini askofu mteule na msaididizi, wajumbe wa baraza kuu mmenisikia kwa maono na toba naamini mnanielewa,” alisema.

Manung’uniko, alisema si chanzo cha baraka na aliwataka wafuate katiba ya kanisa hilo na kusimamia neon la Mungu.

“Hata mlipopita kwenye mawimbi bado hamkuacha kuabudu wapo watu wakiona mawimbi makubwa wanaacha kuabudu asanteni mmelifanya lile Mungu analotaka sameheaneni na msahau yaliyopita,” alisema.

Askofu mstaafu wa kanisa hilo, Mbedule alisema kwa kuwa ameshastaafu atakachokifanya ni kuendelea kuwaheshimu viongozi wa kanisa hilo na kwamba hana kinyongo ya yeyote.

“Sina kinyongo na washariki wala viongozi, nitaendelea kuwaheshimu kikubwa shirikianeni tumewachagua viongozi wapya nashukuru uchaguzi umeisha salama,” alisema.

Alipopewa nafasi ya kuzungumza, Askofu Ngwema aliahidi kuwaunganisha waumini ili kurejesha heshima ya kanisa hilo mkoani Mtwara.

”Nimeupokea wito huu kwa unyenyekevu mkubwa sana kila mwenye mapenzi mema atuombee ilitufanye mapenzi ya mungu iweze kukua na kusonga mbele,” alisema.

Mchungaji Mposola alisema hayakuwa matarajio yake kuwa sehemu ya uongozi wa kanisa hilo na kwamba atafanya kazi kuhakikisha anatekelezwa wito huo wa Mungu.

“Napenda kuona Mungu akinitumia na akinisaidia kufanya vile ambavyo anapenda kwa sababu katikati ya wengi nimeonekana kwa ajili ya kujenga na kusogeza mbele dayosisi yetu,“ alisema.

Erick shumbusho ni katibu na mtunza hazina wa usharika huo, alisema ni imani yao kuwa uchaguzi uliofanyika umewapa kiongozi atakayeendeleza dayosisi hiyo.

“Tunafurahi huduma ya kanisa letu imerejea hata amani imerejea kwetu tunafurahia ilikuwa kelele za miaka mingi tunashukuru kupata kiongozi mpya wa kuongoza dayosisi yetu” alisema Shumbusho.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa tatu wa Sinodi, Francis Mandamo alisema mkutano huo umehudhuriwa na wajumbe 125 kutoka katika majimbo saba yanayounda Dayosisi hiyo.

Aliyataja majimbo hayo ni Magharibi  linalojumuisha  Usharika wa Masasi, Ndanda na Mtandi, Jimbo la Pwani usharika wa Mtwara Magomeni, jimbo la kaskazini linajumuisha usharika wa Lindi mjini, Ingawali  na Nyangao.

Mengine ni Jimbo la Kusini linajumuisha usharika Tandahimba na Newala, Jimbo la Kaskazini Magharlibi linajumuisha usharika wa Nachingwea Ruangwa na Liwale, jimbo la Mtambaswala linajumuisha  Mtambaswala yenyewe na usharika wa Mangaka na Jimbo la Kilwa linajumuisha  usharika wa Kilwa na Somanga.