KLM kuinufaisha Tanzania

Muktasari:

  • Tanzania yatajwa kunufaika katika huduma mpya za malazi kifahari kwa watumiaji wa usafiri wa anga, kutoka katika kampuni ya ndege KLM, wakiwalenga wateja mahususi wa tabaka la uchumi na daraja la biashara.

Dar es Salaam. Tanzania inazidi kunufaika na huduma mbalimbali ndani na nje ya nchi, huku ikitarajiwa kuwa nchi ya kwanza kutoka Afrika, kunufaika na huduma mpya za malazi kwa watumiaji wa usafiri wa anga, kutoka kampuni ya Koninklijke Luchtvaart Maatschappij (KLM) ya Uholanzi.

 Kampuni hiyo imekuja na huduma mpya inayotambulika kama ‘Premium Comfort In’ ambayo ni huduma ya malazi kwa wateja mahususi wa tabaka la uchumi na daraja la biashara.

Huduma hiyo inatajwa kuwepo katika ndege zake za Boeing 777 na 787 ikiwalenga wateja wake mahususi ambao wanataka kufurahia fahari ya safiri hiyo katika chumba hicho kipya.

Akitoa maoni yake kuhusu chumba hicho kipya, Meneja wa Shirika la Air France – KLM nchini Tanzania, Alexander van de Wint, amesema huduma hiyo mpya inaipa ukaribu zaidi KLM kukidhi mahitaji na matakwa ya wasafiri wao.

"Tunafuraha kutambulisha daraja letu jipya la ‘Premium Comfort Cabin’ lenye vyumba vya kifahari,”

“Kwa toleo hili jipya, tunaweza kukidhi mahitaji ya wateja wetu wanaothamini starehe zaidi. Wateja katika jumba hili wanapata pia kufurahia kipaumbele cha anga.” Ameeleza

Amesema, kwa kuanzishwa kwa Premium Comfort, KLM inalenga kukidhi mahitaji yote ya wateja wao katika daraja hilo jipya.