Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

KONA YA MSTAAFU: Ya kale kwa mstaafu hayapo, sasa yamekuwa mapya...

Wajukuu wa mstaafu wetu wa kima cha chini walinipitisha babu yao kwenye tanuru la moto, kwenye kipindi nilichopaswa kuwa nikisherehekea kwa amani miaka 64 ya uhuru wa nchi niliyoshiriki kuijenga mwenyewe!

Wamenipitisha kwenye tanuru la moto kiasi cha kujiona nina miaka 80 tofauti na miaka 67 nilitonato na kujidai nato, kwa hoja na maswali yao yaliyokwenda shule hadi kunifanya nikubali kuwa kweli sasa wajukuu zangu walikuwa na nazo akili  kubwa za kidunu zinazohitaji majibu na siyo bla bla za kizee!

Kwa hakika wamefanya nikumbuke sana mwaka 1975, miaka 50 iliyopita, wakati majirani zetu wa Kongo, wakati huo wa enzi za Rais wao aliyeitwa Mobutu Sese Seko Kuku wa Zabanga na nchi yao ikiitwa Zaire.

Mwaka huo wa 1975, Wakongo hao walituletea mtindo wa kucheza muziki uliotokea kupendwa sana na wapenzi wa muziki barani Afrika, waliouita ‘Kavasha’, uliomfanya mstaafu wetu na wastaafu wenzake wakaribie kuvunja nyonga zao kwa kuupenda na kuucheza kila ulipopigwa!

Mstaafu wetu na wenzake wakiwa ndiyo “matineja”, ‘teen agers’ wakati huo, wanaukumbuka sana wimbo uliopata kupendwa sana ulioitwa na majirani zetu Novelle Generation, wakiongozwa na wanamuziki wao bora miaka hiyo kama vile Vata Mombassa ‘Jujuman’!

Watangazaji wetu wa wakati huo, akina Uncle J, wakatutafsiria kwamba kwa lugha yetu njema ya Kiswahili, wimbo huo ulikuwa na maana ya ‘Kizazi kipya’, yaani sisi “matineja” wa wakati huo wa miaka 50 iliyopita tulikuwa kizazi kipya! Miaka 50 iliyopita huku tukiwa radhi kusifiwa kuwa ni ‘Taifa la Kesho’!

Miaka 50 baadaye, sasa, wajukuu zangu kweli ni ‘Novelle Generation’, japo hawaujui huo wimbo, lakini siyo ‘Taifa la kesho’, na wanasisitiza kuwa wanapaswa kuwa ‘Taifa la leo’ linalowasikiliza kina Fally Ipupa!

Na ndiyo maana wakati huu wa kusherehekea miaka 64 ya uhuru wa nchi niliyoijenga mwenyewe, wamenipitisha kwenye tanuru la moto kwa maswali yao moto na yaliyokwenda shule!

Kwanza, wajukuu zangu ni wafuatiliaji wazuri wa kona ya wastaafu kwa kile wanachokisema kwa busara kabisa kuwa wao ni wastaafu watarajiwa: pamoja na kuwa sasa hivi ni ‘Novelle Generation’, ‘Kizazi kipya’, ambao tofauti na sisi ambao daima tuliona sifa kuwa ‘Taifa la kesho’ lisilofika, wao wanataka kuwa ‘Taifa la leo’ fasta!

Wamekuwa wakinihoji inakuwaje mstaafu wa kima cha chini niliyeijenga nchi kama mimi ninaishia kupata laki moja na elfu hamsini tu kwa mwezi, ya keki ya Taifa niliyoshiriki kuipika, wakati mwakilishi wangu ambaye hakupuliza hata moto kuipika akipokea shilingi... mama wee!... milioni 16 kwa mwezi! Ninaishia kung’aa macho tu bila majibu!

Novelle Generation, kizazi cha sasa, wanajiuliza inawezekanaje kona ya wastaafu, ambayo imetumia nafasi yake tangu mwaka 2021 ilipoanzishwa, kutumia nusu ya makala zake, kama siyo robo tatu ya makala zake kudai nyongeza ya pensheni kwa wastaafu walioshiriki kuipika keki ya Taifa...

...lakini wanapopata nafasi ya kuongea na mheshimiwa kiongozi wa nchi tunaishia kushangilia badala ya kutafuta nafasi ya kuongea na mhusika kuhusu hili. Tunaishia kuwa Novelle Generation ile ya ‘Taifa la kesho’ lisilofika kesho, badala ya kuwa ‘Taifa la leo’ lenye madai yanayoeleweka!

Wajukuu wamefanya babu yao niishie kujisikia kama mzee wa miaka 80 badala ya miaka 67 nilivyo navyo! Wameniambia kuwa tofauti na sisi tulioaminishwa kuwa mtu akikuzaba kofi la shavu la kuume umpe na shavu la kushoto akuzabe tena!

Mawee, kwao ni tofauti. Eti mtu akikuzaba kofi la shavu la kuume humgeuzii shavu la kushoto amalize kazi! Novelle Generation, kizazi na Taifa la leo, wanasema shavu la kushoto hageuziwi mtu... mpaka kieleweke kwanza!

Eti wanaanza kwa kutunyima hata viti kwanza kwenye daladala! Wanaohusika waamke!



0754 340606 / 0784 340606