Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kura zarudiwa tena uchaguzi KKKT


Muktasari:

  • Uchaguzi wa nafasi ya  Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT), unarudiwa kwa awamu wa pili baada ya wagombea wawili wa nafasi kura zao kutokufika theluthi mbili kama kanuni za uchaguzi wa kanisa hilo zinavyotaka.

Arusha. Uchaguzi wa nafasi ya  Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT), unarudiwa kwa awamu wa pili baada ya wagombea wawili wa nafasi kura zao kutokufika theluthi mbili kama kanuni za uchaguzi wa kanisa hilo zinavyotaka.

Mwenyekiti wa uchaguzi huo Askofu Amon Mwenda wa Dayosisi ya Ruvuma, ametangaza tena kurudiwa uchaguzi baina ya wagombea wawili kati ya watatu wa nafasi hiyo baada ya wagombea wote watatu kutokupata theluthi mbili ya kura.

Wagombea hao ni mkuu wa zamani wa KKKT (2007-2015), Askofu Alex Malasusa wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Askofu Abednego Keshomshahara wa Dayosisi ya Kaskazini Magharibi.

Katika uchaguzi wa mara ya pili, Askofu Malasusa amepata kura 142 huku Askofu Keshomshahara akipata kura 96.

Kanuni za uchaguzi za KKKT zinaeleza kuwa mshindi atapatikana kwa kupata kura zisizopungua theluthi mbili ya zote zilizopigwa na iwapo mshindi hatapatikana katika duru la kwanza, majina mawili yaliyopata kura nyingi ndiyo yatakayopigiwa tena kura.

Iwapo theluthi mbili haitapatikana katika duru la pili, kura ya wingi au uchache itatumika kwa duru la tatu ili kumpata mshindi.

Uchaguzi huo unaofanyika usiku huu Agosti 24, 2023, katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira (Tuma), ambapo kwa sasa zoezi la kupiga kura limerudiwa kwa awamu ya pili kati ya Askofu Malasusa na Askofu Keshomshahara.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo wa uchaguzi,katika awamu ya kwanza, kura zilizopigwa ni 253, kati ya hizo Malasusa akipata kuta 90, Keshomshahara kura 83, Fihavango alipata kura 69 na kura 11 zikiharibika.

Kutokana na kura za wagombea kutokufika theluthi mbili, mwenyekiti huyo amesema uchaguzi unarudiwa kwa Askofu Malasusa na Keshomshahara kupigiwa kura tena, ambapo kura zimeshapigwa na zoezi linaloendelea kwa sasa ni kuhesabu kura hizo.

Nafasi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na Askofu Fredrick Shoo ambaye ameiongoza kwa miaka nane.