Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kihongosi awataja Chadema kuhusika katika vurugu, wenyewe wamjibu

Muktasari:

  • Msemaji wa Chadema Brenda Rupia amejibu hoja hizo akisema hazina ukweli wala mashiko yoyote.

Dodoma. Wakati Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikiwatuhumu chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuwa kimeacha ajenda ya siasa na badala yake wamekuwa wanaharakati wa kuhamasisha vurugu na maandamano, chama hicho cha upinzani kimejibu hoja hizo kikisema hazina mashiko wala ukweli.

Akizungumzia na vyombo vya habari jijini Dodoma leo Jumamosi Juni 23,2026, Katibu wa Itikadi, Mafunzo na Uenezi wa CCM, Kenan Kihongosi amesema Chadema kwa sasa kimeacha siasa badala yake limekuwa genge la wanaharakati wa kuhamasisha vurugu na maandamano.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Chadema, Brenda Rupia amejibu shutuma za Kihongosi kwamba hazina ukweli wala mashiko yoyote na wala hakuna ukweli ambao unaweza kusimama katika jambo hilo.

"Kwanza atuambie hao anaosema wanalipwa, nani anawalipa na  kwa kiasi gani hicho kinacholipwa," amesema Rupia.

Hata hivyo, Kihongosi amesisitiza akidai kuwa Chadema kinafadhiliwa na watu wa nje kwa ajili ya kuvuruga amani ya nchi ambayo amesema inaweza kuvurugika kwa sekunde moja, lakini kuijenga ni ngumu.

"CCM tunazo taarifa za uhakika kuwa wenzetu Chadema wamefanya vikao vya siri kwa ajili ya kuhamasisha vurugu na maandamano, wenzetu wana ajenda ya kuvuruga amani ya nchi hii,"amesema Kihongosi.

Mwenezi huyo amesema ni wakati sasa kuwakataa watu wa aina hiyo, kwani hawana jipya na ajenda zao zimekuwa na matukio huku wakitoa matusi kwenye mkutano ya hadhara ambayo si utamaduni wa Mtanzania wala miongozo kwa vyama vya siasa.

Amewataka vijana na wanawake kuacha kurubuniwa kwani wanaowarubuni wao na watoto wao wako nje ya nchi wakilipiwa na kusomeshwa na watu wengine huku wao wakiwa ndani ya nchi nao wanalipwa ili kuchochea vurugu.

"Wengine wako nje na walishaukana uraia wa Taifa lao, leo wanahamasisha vijana kufanya maandamano wakati hakuna ndugu zao hata mmoja kwenye maandalizi hayo," amesema.

Amesema tayari CCM kimetoa taarifa kwa vyombo vya ulinzi na usalama kwa ajili ya kuzuia matukio hayo na kuwaomba wananchi waendelee kutoa taarifa kila wanapobaini kuna mambo kama hayo ili yazuiwe mapema.

Katika hatua nyingine Kihongosi amesema bado anatamani kukutana kwenye mdahalo na viongozi wa Chadema aliowataja kuwa ni John Heche (Makamu Mwenyekiti Bara), Godbless Lema, Boniface Jakob na Joseph Mbilinyi (Sugu) akisisitiza waende pamoja wakati yeye atakuwa peke yake.

Amesema Chama cha Mapinduzi kinajua kupika viongozi kama ilivyo kwake yeye aliyepitia maeneo na nafasi mbalimbali ambazo viongozi wa Chadema hawatamuweza.

Amewataka Watanzania kuandamana katika kujenga uchumi wa Nchi ili kila mtu asimame katika eneo lake la kuzalisha mali na kuacha Matendo ya ubaguzi.

Kuhusu CCM amesema ni chama kilichoendelea kujijengea imani kwa wananchi na kimekita mizizi hadi ngazi ya chini ndiyo maana kinaendelea kuaminika na kuchahuliwa.