Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kauli ya Kihongosi yamuibua Lema na Sugu, yeye asema

Muktasari:

  • Kihongosi amesema anawataka Makamu Mwenyekiti wa Chadema- Bara, John Heche, mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho, Godbless Lema na wenyeviti wa kanda, Joseph Mbilinyi maarufu Sugu (Nyasa) na Boniface Jacob maarufu Boni Yai wa Pwani ili wachuane.



Arusha. Kauli ya Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Kenani Kihongosi ya kutaka mdahalo wa wazi na viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) imeibua mjadala huku vigogo hao wa upinzani wakimjibu.

Kihongosi amesema anawataka Makamu Mwenyekiti wa Chadema- Bara, John Heche, mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho, Godbless Lema na wenyeviti wa kanda, Joseph Mbilinyi maarufu Sugu (Nyasa) na Boniface Jacob maarufu Boni Yai wa Pwani ili wachuane.

Mjadala mtandaoni baada ya kauli hiyo umeshika kasi huku Sugu na Lema wakimjibu, wananchi wakimshabulia huku yeye mwenyewe (Kihongosi) akiibuka tena na kusisitiza anawahitaji viongozi hao wachuane kwenye mjadala wa wawazi.

Mbali na Sugu na Lema kumjibu, wachangiaji wengine mtandaoni walisema wangependa kuona mdahalo huo ukifanyika mubashara, mwingine akidai Kihongosi anaitumia Chadema kujijengea umaarufu.

Baadhi wakimshauri aachane na viongozi hao wakidai siyo kiwango chake kisiasa huku wengine wakimtaka kwanza akapime nguvu na viongozi wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha) kabla ya kuwataka viongozi hao.

Juni 5, 2026, Kihongosi akizungumza na wananchi viwanja vya Kanisa Katoliki Ngaramtoni, wilayani Arumeru, mkoani Arusha, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake mkoani Arusha, amesema yuko tayari kwa mdahalo.

“Namtaka Heche aje hapa kushoto, Lema aje hapa kulia, Boni Yai asogee hapa na Sugu wa Mbeya akae hapa. Wote wawepo hao wanne, mimi niwe peke yangu halafu tuanze mdahalo,” amesema Kihongosi.

Kauli hiyo iliibua mjadala huku Lema ambaye ni mbunge wa zamani wa Arusha Mjini, aliandika katika ukurasa wake wa Instagram akimweleza akafanya mjadala na Mbunge wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mohamed Simai Said na Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba.

"Kafanye mdahalo na Simai na Mwigulu. Tittle ya mdahalo iwe namna ya ku-deal na Yuda ndani ya Bunge," ameandika Lema.

Juni 2, 2026, akichangia bajeti ya Wizara ya Fedha ya mwaka 2026/27, Simani aliibua madai bungeni ya uwepo wa mtu serikalini ambaye alimwita ni Yuda anayemsaliti Rais Samia Suluhu Hassan. Simai hakumtaji jina zaidi ya kusema ni Yuda.

Kwa upande wake, Sugu ambaye amewahi kuwa mbunge wa Mbeya Mjini ametoa majibu kupitia ukurasa wake wa Instagram.

“Mwambieni huyu dogo aache ganja hazimfai.”

 Aidha, katika majibu ya Sugu aligusia matukio ya Oktoba 29, 2026 yaliyosababisha mauaji ya wananchi.

Mwingine, jumashabani2150 yeye ameandika: “Uyu jamaaa anatingisha meza ya vinywaji vya gharama😂😂 kaka wale hawawezi.”

Huku elvismangowi  akisema Uliowataja hamna saizi yako hata mmoja,

Jana Jumamosi, Juni 6, 2026, Kihongosi alirejea tena suala hilo alipokuwa akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Soko la Kilombero jijini Arusha, akisisitiza siasa zinapaswa kuendeshwa kwa hoja badala ya matusi.

"Hawa tumewazaa 1992, sisi tumezaliwa 1977, huwezi kutulinganisha. Jana nimewaambia pale Arumeru kwamba nahitaji mdahalo aje Heche, aje Lema, aje Sugu hapa, mimi niwe peke yangu. Leo nimewaona wote wananishambulia mitandaoni, nasema tena nawataka waje kwenye mdahalo," amesema Kihongosi.

"Sisi CCM anatembea mwenezi peke yake, wao wanatembea chama kizima, Kamati Kuu nzima, sekretarieti nzima, jumuiya zote na bado tunawagonga dozi," amesema.

Kihongosi amesema baadhi ya watu wamemshauri viongozi anaowataka ni wakubwa kuliko yeye kisiasa, lakini akasisitiza hana wasiwasi wowote wa kukutana nao katika mdahalo.

"Wamesema kijana nenda hao ni size yako, sisi tujenge nchi. Lakini nasema tena, nawataka kwenye mdahalo," amesema

Katika kusisitiza hilo, Kihongosi amesema:"Nasema tena nawataka waje kwenye mdahalo. Sisi CCM anatembea mwenezi peke yake wao wanatembea chama kizima, kamati kuu nzima, sekretarieti nzima, jumuiya zote na bado tunawagonga dozi."

"Leo mitandaoni ni makelele wanasema ukisikia mlio kwenye chumba cha sindano ujue sindano imefanya nini? na bado, huwezi kujilinganisha na chama kikubwa hiki wala hakijitangazi ndiyo chama kikubwa watu wanajua kwamba hili dude ni kubwa na lina mizizi imetapakaa kila sehemu," amesema.

"Wanajua kwa hiyo mkawaambie hivi mwenezi amesema anawataka tena kwenye midahalo msikimbilie instagram. Yaani kuna watu wanaamini wanaweza kututisha, yaani wale jamaa kweli watutishe sisi. Lema kweli atutishe sisi, Sugu yeye naye atutishe tumuogope, Heche huyu,” amehoji Kihongosi.

Amesema ni muhimu kushindana kwa hoja siyo matusi.

"Wengine huko wamenitukana wameandika matusi kabisa,sasa mimi hakuna kitu napenda kama kutukanwa yaani nafurahi kweli, ukitukana nasikia raha, ndiyo maana tunasema hatunywi sumu hatujinyingi CCM mbele kwa mbele..."amesema.

Huku akiendelea kuimba nyimbo za chama hicho Kihongosi amesema:"Nyimbo tu wanatetemeka, hawa jamaa vipi na hawawezi kweli na ninasema hapa tunawasubiri 2030 waje waseme wamefanya nini na sisi tuseme tumefanya nini tukutane uwanjani.

"Ukihubiri matusi utavuna matusi, ukipeleka maendeleo utavuna maendeleo sasa tutakutana, wanajua hawatuwezi zaidi walete propaganda na kufanya fujo basi,na hizi fujo Watanzania wameshachoka," amesema.