Lady Gaga kumpa Sh1 bilioni atakayewapata mbwa wake waliopotea

New Content Item (2)
Lady Gaga kumpa Sh1 bilioni atakayewapata mbwa wake waliopotea

Muktasari:

  • Mwanamuziki Lady Gaga ametangaza donge nono la Dola 500,000 za Marekani (Sh1.1 bilioni) kwa mtu yeyote atakayesaidia kupatikana kwa mbwa wake wawili, Koji na Gustav.

Marekani. Mwanamuziki Lady Gaga ametangaza donge nono la Dola 500,000 za Marekani (Sh1.1 bilioni) kwa yeyote atakayesaidia kupatikana kwa mbwa wake wawili, Koji na Gustav.
Taarifa hiyo ameitoa leo Jumamosi Februari 27, 2021 katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram akibainisha kuwa mbwa hao walichukuliwa siku mbili zilizopita huko Hollywood.
Taarifa hiyo iliambatanishwa na picha ya mbwa hao ikifafanua kuwa kama kuna mtu ambaye amewanunua au kuwapata atamlipa kiasi hicho cha fedha.
“Nitaendelea kuwapenda kwa kuwa mlihatarisha maisha yenu kwa ajili ya kulinda familia yetu. Daima nyinyi ni mashujaa,” ameeleza mwanamuziki huyo akiwamwagia sifa mbwa wake hao.