Lissu abadili vazi njiani akienda Temeke

Muktasari:

Dakika chache baada ya kuwasili nchini akitokea Ubelgiji alikokuwa akiishi, Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu amebadili vazi lake akiwa njiani kwenda Temeke utakapofanyika mkutano wa hadhara

Dar es Salaam. Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu aliyewasili nchini dakika chache zilizopita akitokea Ubelgiji alikokwenda tangu mwaka 2020, amebadilisha mavazi yake akiwa njiani kwenda katika mkutano wa hadhara unaotarajiwa kufanyika mkutano wa hadhara.

Lissu amewasili nchini leo, Januari 25, 2023 alifika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, akiwa amevalia kombati ya kaki ‘gwanda’ ambalo ni vazi linalokitambulisha chama hicho kwa wafuasi wake.

Hata hivyo mwanasiasa huyo machachari akiwa ndani ya gari alionekana amebadili vazi hilo na kuvalia fulana ya mikono mirefu yenye rangi zinazoakisi bendera ya chama hicho.

Mara baada ya kubadili vazi hilo, Lissu aliendelea kuwasalimia watu katika kila eneo alilokuwa akipita akiwa juu ya gari.

Lissu awasili Tanzania, mamia wampokea

Wafuasi na wapenzi wa chama hicho walikuwa wakishangilia kila alipopita kiongozi huyo huku wengine wakiungana na msafara wake kuelekea katika viwanja vya Bulyaga vilivyopo Wilaya ya Temeke akapokaribishwa kwenye mkutano wa hadhara na kuwahutubia wafuasi na wanachama wa Chadema