Lissu amteua Lema kuwa wakala wake uchaguzi Chadema
Dar es Salaam. Mgombea uenyekiti wa Chadema Taifa na makamu mwenyekiti anayemaliza muda wake, Tundu Lissu, amemteua Godbless Lema kuwa wakala wake katika uchaguzi unaofanyika leo.
Kuteuliwa kwa Lema, ambaye si mjumbe wa mkutano mkuu kwa sasa, kumetangazwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika, leo Jumanne, Januari 21, 2025 katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.
Akitoa tangazo hilo muda mchache kabla ya uchaguzi huo kuanza, Mnyika amesema suala hilo halivunji kanuni za uchaguzi.
Endelea kufuatilia Mwananchi.