Lucky Dube akumbukwa

Aliyekuwa mwanamuziki mashuhuri duniani, Lucky Dube wakati wa uhai wake

Muktasari:

“Leo tunatoa heshima zetu kwa mwanamuziki huyu, muziki wake uliwaguza mamilioni ya watu duniani,” amesema

Mthethewa aliendelea na kumpongeza Dube akisema kuwa muziki wake ulianza tangu kipindi cha Apartheid.

Siku kama ya leo, Oktoba 18 mwaka 2007, mwanamuziki mashuhuri duniani, Lucky Dube alifariki dunia. Katika kumbukizi ya kifo hicho, Waziri wa Sanaa na Utamaduni, Natji Mthethwa amewataka raia wa Afrika Kusini kumkumbuka mwanamuziki huyo kwa kumuombea.

“Leo tunatoa heshima zetu kwa mwanamuziki huyu, muziki wake uliwaguza mamilioni ya watu duniani,” amesema

Mthethewa aliendelea na kumpongeza Dube akisema kuwa muziki wake ulianza tangu kipindi cha Apartheid.

Dube aliuawa kwa kupigwa risasi eneo la Rosettenville, Johannesburg.

Kwa habari zaidi nunua gazeti la Mwananchi kesho au waweza kusoma kwa kupitia mtandao 'Mwananchi epaper' Bonyeza hapa