Lulu na Majizo wafunga ndoa

Tuesday February 16 2021
Lulu pic

Dar es Salaam. Baada ya uchumba uliodumu kwa takribani miaka miwili, msanii wa filamu nchini Tanzania, Elizabeth Michael maarufu Lulu amefunga ndoa na Francis Ciza ‘Majizo’ ambaye ni mkurugenzi wa kituo cha televisheni cha tvE na redio EFM.

Ndoa hiyo imefungwa leo Jumanne Februari 16, 2021 katika kanisa la St Gasper lililopo Mbezi  Beach Jijini Dar es Salaam.

Harusi hiyo imefungwa kwa siri bila shamrashamra tofauti na ndoa za wasanii mbalimbali nchini ikielezwa kuwa waliohudhuria ni ndugu wachache.

Advertisement