Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ma-DC walia na michango holela shuleni

Kilosa. Wakati shule zikifunguliwa, baadhi ya wakuu wa wilaya wamekemea tabia ya wakuu wa shule kuanzisha michango kwa wanfunzi bila kufuata utaratibu.

Miongoni mwa viongozi hao ni Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Alhaj Majid Mwanga ambapo akizungumza na wananchi wa kata ya Msowero leo Januari 10, amesema kumezuka tabia ya walimu kuwatoza wazazi fedha za michango kwa madai kuwa shule zina uhitaji jambo alilosema halina ukweli wowote.
Kauli ya DC Mwanga imekuja wakati kukiwa na barua iliyosambaa mitandaoni ikionesha michango ya Shule ya Sekondari ya wasichana Dakawa iliyomo wilayani humo bila kibali cha ofisi yake.
“Mkuu wa shule hii anajua tayari Serikali ilishatoa fedha zaidi ya Sh1 milioni kwa ajili ya ujenzi huo," amesema Alhaj Mwanga.
Kufuatia kusambaa kwa barua hiyo mkuu huyo wa wilaya amesitisha michango hiyo na ameagiza Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) kuchunguza mara moja akaunti ya shule hiyo kujua kiasi gani cha fedha ambacho kimechangishwa na Mwalimu Mkuu huyo hadi sasa.
"Kama kuna uhitaji wa kuwashirikisha wazazi kuchangia kitu chochote mkuu wa shule usichangishe michango hiyo mpaka upate kibali kutoka kwangu mimi mkuu wa wilaya, haijalishi hata kama wazazi wameridhia mimi ndio natoa kibali na hili nataka wakuu wote wa shule za msingi na sekondari mlijue," amesema Alhaj Mwanga.
Amesema Serikali inatekeleza Sera ya elimu bila malipo kuanzia darasa la awali hadi kidato cha sita na michango yote ambayo itachangishwa lazima iwe na kibali kutoka kwangu mkuu wa wilaya husika na sio mtu mwingine.
Kwa upande mwingine, Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Said Mtanda amefuta baadhi ya michango ambayo wanafunzi wanaoripoti kidato cha kwanza katika jiji la Arusha, walitakiwa kuchanga.
Licha ya kufuta michango hiyo, Mkuu huyo wa wilaya ametoa siku saba wazazi kuwapeleka shule walizopangiwa watoto wao waliofaulu kidato cha kwanza la sivyo msako mkali utaanza ili kuwachukulia hatua.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Januari 9, mara baada ya kikao cha wakuu wa shule, waratibu elimu Kata na maafisa elimu na watendaji katika jiji la Arusha, Mtanda alisema amebaini kila shule ilikuwa imeandika michango kwa wanafunzi wapya.
“Nimebaini kila shule katika fomu za kujiunga walikuwa na michango yao na taratibu mbali mbali, ikiwepo kutoza faini ya tofali 50 kwa mwanafunzi atakayeruka ukuta, sasa nimesema hapana tuwe na mfumo unaofanana,” amesema.
Amesema baada ya kupitia fomu za shule zote, wamekubaliana na kuwa michango inayofanana kwa jiji zima na amezitaka shule kuita kikao na wazazi kukubaliana.
“Kwa kuwa michango mingi ilipitishwa na wazazi sasa tumepunguza baadhi ya maeneo na kuondoa mingine lakini lazima wazazi wakutane na viongozi wa shule na kukubaliana,” amesema
Amesema Rais Samia Suluhu ametoa maelezo kuhakikisha michango isiyo na tija iondolewe ili kutokwamisha wazazi kupeleka watoto shule hasa baada ya kuwepo mfumo wa elimu bila malipo.