Maandalizi harusi ya Mrema yakamilika

Muktasari:

  • Maandalizi kwa ajili ya harusi ya Mwenyekiti wa chama cha Tanzania Labor Part (TLP), Agustino Mrema tayari yamekamilika tayari wamewasili katika kanisa katoliki parokia ya Uwomboni Kiraracha mkoani Kilimanjaro.


Moshi. Maandalizi kwa ajili ya harusi ya Mwenyekiti wa chama cha Tanzania Labor Part (TLP), Agustino Mrema tayari yamekamilika tayari wamewasili katika kanisa katoliki parokia ya Uwomboni Kiraracha mkoani Kilimanjaro.

Mrema ambaye aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini, kuwa mbunge na kugombea urasi wa Tanzania, leo Alhamisi Machi 24, 2022 anafunga tena ndoa baada ya mke wake kufariki mwaka jana.

Hali ilivyo eneo hilo.

Mrema alikuwa wa kwanza kutoka nyumbani kwake na kuingia kwenye gari na baadae akatoka bibi harusi akiwa amejifunika kanga hadi usoni ili asionekane na watu.

Hata hivyo waandishi wa habari walitaka kumuona lakini mzee mmoja wa kichaga aliyekuwepo eneo hilo, amesema mila za kichaga zinamtaka atoke akiwa amejifunika.

VIDEO: Sababu za Mrema kutaka kuoa

Mwenyekiti wa chama cha Tanzania Labor Part (TLP), Agustino Lyatonga Mrema ameelezea kilichomsukuma kuoa kuwa ni pamoja na kuepuka matamanio na kuzini kwa macho. Soma zaidi