Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mabasi yaanza safari yakichelewa kwa saa sita mkoani Songwe

Muktasari:

  • Hatimaye Mabasi yanayofanya safari ya kutoka Tunduma mkoani Songwe kuelekea mikoa ya Mbeya, Iringa, Sumbawanga, Dodoma, Arusha, na Dar es salaam yameanza safari zake leo Februari 23, 2022 mchana baada ya malori yaliyofunga njia eneo kubwa la barabara ya kuelekea Tunduma kusogezwa.

Songwe. Hatimaye Mabasi yanayofanya safari ya kutoka Tunduma mkoani Songwe kuelekea mikoa ya Mbeya, Iringa, Sumbawanga, Dodoma, Arusha, na Dar es salaam yameanza safari zake leo Februari 23, 2022 mchana baada ya malori yaliyofunga njia eneo kubwa la barabara ya kuelekea Tunduma kusogezwa.

Kwa siku tano eneo la Tunduma lilijaa malori na usiku wa kuamkia leo Jumatano Februari 23, 2022 yamefunga barabara na kusababisha magari mengine kukwama.

Akizungumza mmoja ya wakatisha tiketi za mabasi ya mikoani katika stendi ya Vwawa Ofisi za New Force ambaye hakutaka jina lake kuwekwa wazi amesema kawaida mabasi hayo yanapita Vwawa saa 12.20  asubuhi lakini leo yamechelewa kuliko kawaida  kwa vile yamepita Vwawa saa 6.00 mchana.

Amesema abiria hawakuwa wasumbufu kutokana na tatizo lililojitokeza linaeleweka na haikuwa sababu ya upande wao wasafirishaji. 

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Omary Mgumba amesema msongamano huo ulitokana na malori kuwa mengi na barabara kuwa finyu

Amesema changamoto hiyo inahitaji kusuluhishwa kwa kujenga njia nne za barabara kuanzia Mlowo hadi Tunduma