Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Madaktari bingwa JKCI kuweka kambi Hospitali ya Kanda Chato

Muktasari:

Watu walio na matatizo ya moyo mikoa ya kanda ya ziwa wanatarajia kunufaika na kambi siku tano ya madaktari bingwa itakayofanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Chato

Dar es Salaam. Kambi ya siku tano inatarajiwa kufanywa na madaktari bingwa kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya kikwete (JKCI) wakishirikiana na madaktari wataalamu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato (CZRH) kati ya Aprili 15 hadi Aprili 19, 2024.

Kuendeshwa kwa kambi hiyo kunalenga kuwapunguzia wananchi wa mikoa ya Geita, Kagera, Kigoma, Shinyanga, Mwanza na Mara adha ya kufuata huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo mbali.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Habari Uhusiano na Mawasiliano, Husna Karamagi madaktari wanatarajia kuendelea kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya magoniwa ya moyo kwa wananchi wa mikoa hiyo.

“Huduma hizi za kibingwa za uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo pamoja na mishipa ya damu zitatolewa kwa watu wa rika zote, yaani watoto na watu wazima,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Hilo linafanyika ikiwa ni jitihada za kuendelea kutekeleza azma ya uanzishwaji wa Hospitali ya Kanda ya Rufaa ya Chato kama taasisi ya moyo inayojitegemea katika kanda ya ziwa.

“Hospitali inaendelea kutekeleza azma hii ikiwa ni pamoja na utoaji wa huduma endelevu za magonjwa ya moyo kwa kiwango cha juu. Huduma hizi zinatolewa kwa kushirikiana na JKCI kwa kuleta madaktari bingwa bobezi dani ya Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato (CZRH) kwa kipindi cha miaka mitano (5),” imeeleza tsarifa hiyo.

Taarifa hiyo inabainisha watakaogundulika kuwa na matatizo ya moyo watafanyiwa uchunguzi zaidi na kupatiwa matibabu hapohapo.

Shughuli hiyo ni muendelezo wa kuwapunguzia wananchi wa kanda ya ziwa adha ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma.

“Wananchi mnaombwa kujitokeza kupima afya zetu kujua kama tuna matatizo ya moyo ili kuanza matibabu mapema kwa wataogundulika kuwa wagonjwa,” imeeleza taarifa hiyo.