Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Madaktari washangaa kumuona Lissu akiwa hai -VIDEO

Muktasari:

  • Ni baada ya mbunge huyo wa Singida mashariki kufikishwa hospitalini hapo akiwa anavuja damu nyingi

Dar es Salaam. Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa amesema madakatari nchini Kenya wameshangazwa kumwona Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu akiwa hai kutokana na shambulio la risasi lililotokea Septemba 2017 mjini Dodoma.

Msigwa aliyekuwa miongoni mwa viongozi wa Chadema waliomsafirisha Lissu kutoka Dodoma siku hiyo kwenda jijini Nairobi, aliliambia gazeti hili jana kwamba Lissu alivuja damu nyingi na kama asingepata huduma ya haraka angefariki.

“Tulipofika Nairobi, madaktari walishangaa kuona Lissu akiwa hai, kwa sababu alipoteza damu nyingi sana. Lakini niwashukuru sana madaktari wa hospitali ya Dodoma General kwa huduma waliyotoa kufanya Lissu tufike Nairobi,” amesema Mchungaji Msigwa na kuongeza:

“Nataka tu niwaambie Watanzania kwamba Tundu Lissu wetu aliumizwa sana katika jaribio la kuchukua uhai wake. Watu wasichukulie kama ni jambo dogo, ni jambo kubwa lililoharibu hata akili za watu tuliokuwa karibu naye.” Soma Zaidi