Madiwa watakiwa kusimamia ujenzi madarasa Iringa

Muktasari:

  • Madiwani mkoani Iringa wametakiwa kusimamia miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa inayotekelezwa katika halmashuri zao kwa kufika eneo la ujenzi.

  


Iringa. Madiwani mkoani Iringa wametakiwa kusimamia miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa inayotekelezwa katika halmashuri zao kwa kufika eneo la ujenzi.

Ombi hilo limetolewa leo Alhamisi Novemba 25, 2021 na mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM, Salim Abri wakati akizungumza na madiwani wa mkoa huo katika ukumbi wa Royal Pulm Mjini hapo.

Salim amesema fedha zilizotolewa kutokana na Mpango wa maendeleo kwa ustawi wa taifa na mapambano dhidi ya Uviko -19 lengo ni kusaidia sekta ambazo zimethirika kutokana na janga la ugonjwa huo.

“Fedha zilizotolewa ni kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na si miradi mingine hivyo madiwani mkasimamie ujenzi huo madarasa yajengwe katika kiwango kinachostahili na yakabidhiwe kwa wakati” amesema.

Mkoa wa Iringa ulipokea kiasi cha Sh8.6 bilioni ambazo zimeelekeza katika afya elimu na utalii.

Naye, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa, Ibrahim Ngwada amesema Sh660 milioni zimetengwa kwa ajili ya umaliziaji wa madarasa 23.

Aidha amesema kuwa mkoa huo umepata Sh700 milioni kwa ajili ya ujenzi wa wodi katika hospitali ya wilaya ya Frelimo, Sh600 milioni kwa ajili ya ujenzi wa Machinjio ya Ngelewara.

Kwa upande wake Katibu tawala wa Mkoa huo amesema mkoa umepata Sh4.9 bilioni katika elimu ambapo itaenda kuongeza vyumba vya madarasa kwa shule za sekondali na msingi.