Madiwani wataka wafanyabishara wa vyuma chakavu wadhibitiwe

Muktasari:
- Imeelezwa kuwa biashara ya vyuma chakavu inayoendelea imekuwa chanzo cha uharibifu wa miundombinu na wizi wa vifaa vya majumbani.
Songwe: Imeelezwa kuwa biashara ya vyuma chakavu inayoendelea imekuwa chanzo cha uharibifu wa miundombinu na wizi wa vifaa vya majumbani.
Hayo yamesemwa leo Ijumaa Oktoba 29, 2021 na Madiwani wa halmashauri ya Mbozi Mkoani Songwe, kuwa inahitajika mikakati ya kudhibiti wafanyabiashara wa vyuma chakavu.
Ikibainika wafanyabaishara hao wanauza vifaa vipya hatua kali zichukuliwe dhidi yao.
Diwani wa kata ya Vwawa, George Kiwaya amesema uuzwaji wa vifaa hivyo umesababisha watoto kuiba vifaa majumbani vyenye asili ya chuma.
"Katika hili naomba madiwani wenzangu waniunge mkono tuwe na azimio ili vyombo vya dola viongeze udhibiti wa biashara hiyo" amesema Kiwaya.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri ya Mbozi, George Msyani amekiri kuwapo na uharibifu unaosababishwa na uuzaji wa vyuma chakavu ambao pia umechangia kuporomosha maadili ya watoto.