Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Magari yenye namba ya usajili ya Zanzibar halali kutumia bara

Muktasari:

  • Kwa sasa magari au trela zenye namba za usajili wa Tanzania Bara ni halali kutumika Tanzania Zanzibar.

Dar es Salaam. Huenda magari na trela zilizosajiliwa kwa namba za usajili za Zanzibar yakaruhusiwa kutumika Tanzania Bara, baada ya Serikali kupendekeza mabadiliko ya Sheria ya Usalama Barabarani Sura ya 168.

Utekelezwaji wa hilo, unategemea ridhaa ya wabunge juu ya pendekezo la mabadiliko ya sheria hiyo lililotolewa na Serikali kupitia bajeti yake ya mwaka wa fedha 2026/27.

Kabla ya pendekezo hilo, Sheria ya Usalama Barabarani ya sasa, inazuia magari au trela zenye namba za usajili za Zanzibar kutumika Tanzania Bara huku zilizosajiliwa Tanzania Bara zikiruhusiwa Zanzibar.

Pendekezo hilo, limetolewa bungeni jijini Dodoma leo, Alhamisi Juni 11, 2026 na Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omar, alipowasilisha Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2026/27.

Amesema Serikali inapendekeza marekebisho ya sheria hiyo ili kuruhusu gari au trela iliyosajiliwa kwa mujibu wa sheria za usajili za Tanzania Zanzibar kutumika Tanzania Bara.

Hata hivyo, pendekezo hilo limeweka msisitizo, magari au trela hizo ziruhusiwe kutumika pale ambapo kodi zote kwenye gari au trela husika zimelipwa kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizopo.

“Kwa sasa utaratibu huu unatumika kwa magari yanayotoka Tanzania Bara kwenda Tanzania Zanzibar,” amesema.

Amesema lengo la hatua hiyo ni kutatua changamoto zilizopo kwenye matumizi ya vyombo hivyo, baina ya pande mbili za Muungano pasi na kuathiri mapato ya Serikali.