Magufuli amsimamisha Mkurugenzi wa TIC

Aliyekuwa  Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji (TIC), Julieth Kariuki .

Muktasari:

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Biashara na Uwekezaji, Profesa Adolf Mkenda inasema kuwa utenguzi wa kiongozi ulianza Aprili 24 mwaka huu.

Dar es Salaam. Rais John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji (TIC), Julieth Kariuki kwa sababu mbalimbali ikiwemo kutochukua mshahara wake tangu alipoteuliwa Aprili, 2013.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Biashara na Uwekezaji, Profesa Adolf Mkenda inasema kuwa utenguzi wa kiongozi ulianza Aprili 24 mwaka huu.

Kairuki anakuwa kigogo wa pili wa mashirika ya umma kutenguliwa au kusimamishwa mara baada ya Dk Magufuli kumsimamisha Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dk Ally Simba mapema wiki hii

Kairuki ambaye ni mwanasheria na mtaalamu wa masuala ya ubia kati ya Serikali na wawekezaji, aliteuliwa katika nafasi hiyo na Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete kutoka katika chama cha mabenki Afrika Kusini akiwa ni Meneja Mkuu wa idara ya benki na huduma za fedha.

Uchambuzi wa kina utafuta katika gazeti…