Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maisha ya Putin utotoni, familia na ujasusi

Rais wa Russia, Vladimir Putin (kulia) akiwa na Rais wa Marekani, Joe Biden. Picha na Maktaba

Muktasari:

Toleo lililopita tuliona mzozo ulioko kati ya NATO na Russia. Lakini kwa kutazama kwa makini sana, aliyeko nyuma ya mzozo huo ni mwanadamu anayeitwa Vladmir Putin, ambaye hadithi ya maisha yake ni ya kusisimua.

Baba yake, Vladimir Spirdonovich Putin, alikuwa amejitolea kufanya kazi katika manowari kupigana dhidi ya Wajerumani katika Vita Kuu II. katika nchi ya Estonia barani Ulaya.

Wafuasi wa adui waliposaliti kundi lake, aliepuka kukamatwa kwa kujizamisha kwenye kinamasi na kupumua kupitia mwanzi.

Miongoni mwa wanaume 28, ni yeye tu na wengine wanne walionusurika kifo. Aliporudishwa vitani, aliamriwa kumkamata askari wa Ujerumani kwa mahojiano.

Alitambaa ardhini kwa ukaribu kadiri alivyoweza kufika kwenye eneo la alilokuwa adui, lakini ghafla Mjerumani akamwona na kurusha guruneti.

Vipande vya vyuma na mawe vilivyotokana na mlipuko huo vilimjeruhi vibaya miguu yake.

Saa kadhaa baadaye, mwenzake mmoja alimbeba na kuvuka naye Mto Neva uliokuwa na barafu na kumfikisha kwenye hospitali pekee iliyokuwapo.

Wakati huohuo, mama yake Putin, Maria, alinaswa katika katika jiji la Leningrad lililozingirwa na jeshi la Ujerumani.

Maria aliolewa na Vladimir Spirdonovich alipokuwa na umri wa miaka 17. Alikuwa na elimu duni na hakuwa na ujuzi wa jambo lolote la kitaaluma.

Wajerumani walipojaribu kuliteka jiji hilo kupitia kampeni ya mashambulizi na mabomu ambayo yaliendelea kwa karibu miaka mitatu, alianza kushindwa na silaha ya adui wa kimya kimya yaani njaa.

Mara moja, aliamka akiwa amelala kando ya safu ya maiti. Alikuwa amezimia barabarani kutokana na njaa na kudhaniwa kuwa amekufa.

Alikwenda kumtafuta mume wake na kumkuta hospitalini akiwa amepona majeraha yake.

Alipoona alivyodhoofika kwa kukonda, mumewe alimpa chakula chake kwa siri wakati alipokuwa akimtembelea hospitalini kila siku hadi madaktari walipomkamata akiwa naye ameanza kudhoofika kwa kukonda na kumwamuru aache.

Kufikia mwishoni mwa vita, nyumba yao huko Leningrad ilikuwa imeharibiwa na Wajerumani, na walikuwa wamepoteza watoto wawili: mmoja wakati wa utoto, na mwingine kutokana na ugonjwa wa koo unaoambukiza ambao husababisha kupumua kwa shida (dondakoo) ambao uliua maelfu ya watoto wa Leningrad.

Wakati huu Maria alikuwa na umri wa miaka 41 alipojifungua mtoto Vladimir Jumatano ya Oktoba 1, 1952. Alimbatiza kwa siri katika imani ya Othodoksi ya Urusi.

Alimficha hata mumewe kwa sababu alikuwa katibu wa Chama cha Kikomunisti cha katika kitongoji chao. Katika Muungano wa nchi za Kisovieti za Urusi (USSR), mazoea ya kidini yalikatazwa.

Vladimir Putin alikuwa sehemu ya kizazi cha pili cha kuzaliwa katika USSR. Iliundwa Jumamosi ya Desemba 30, 1922 ikiwa ni muungano wa jamhuri 15 za Kisoshalisti za Kisovieti, ikiwamo Russia yenyewe ambayo ilikuwa ndicho kitovu cha Muungano huo kwa sababu ilikuwa na robo tatu ya eneo la Muungano wenyewe.

Mipaka ya Urusi inafika Norway, Finland, Estonia, na Latvia upande wa kaskazini-magharibi; Belarusi na Ukraine upande wa magharibi; Georgia, Azerbaijan, na Kazakhstan upande wa kusini-magharibi; na Uchina, Mongolia, na Korea upande wa kusini-mashariki, na kuifanya kuwa nchi kubwa zaidi ulimwenguni.

Leningrad, jiji ambalo familia ya Putin iliishi, lilikuwa limeitwa St. Petersburg. Lilianzishwa mwaka 1703 na Petro Mkuu kama mji mkuu wa milki ya Kirusi, jiji hilo liliitwa Petrograd wakati wa Vita Kuu ya Kwanza Dunia.

Ilibadilishwa jina na kuitwa Leningrad baada ya mwaka 1924 kwa heshima ya Vladimir Ilyich Lenin, kiongozi wa Mapinduzi ya Kirusi. Mwaka 1991, kutokana na kura ya maoni, jiji hilo lilibadilishwa jina na kuitwa St. Petersburg.


Maisha ya familia yake

Kabla ya vita, baba yake Putin alifanya kazi katika zana za kiwanda cha treni na alikuwa akilipwa vizuri kulingana na viwango vya USSR ambavyo viliruhusu kina Putin kuishi katika nyumba ndogo ambayo walikuwa wakiishi na familia nyingine.

Ili kuongeza kipato cha familia, Maria alifanya kazi mbalimbali. Alifanya kazi kama mlinzi wa nyumba, alifanya vibarua vya kubeba bidhaa za madukani usiku kama mikate na hata kufanya usafi kwenye nyumba za watu.

Katika kitabu cha wasifu wa Putin, aliyewahi kuwa mwalimu wake, Vera Dmitrievna Gurevich, anakaririwa akisema: “Walikuwa na nyumba mbaya. Ilikuwa ya jumuiya ... Hakukuwa na maji ya moto, hakuna bafu. Choo kilikuwa cha kutisha.”


Putin na shule

Alipoanza shule, Putin alifanya vizuri shuleni. Katika daraja la tisa, alichaguliwa kuhudhuria Shule ya Leningrad No. 281, shule ya wanafunzi waliokuwa na akili zaidi zaidi wa jiji hilo.

Ingawa shule hiyo ilibobea katika sayansi, Putin alivutiwa na masomo ya sanaa kama vile fasihi na historia. Wanafunzi wenzake na walimu walimkumbuka kama mwanafunzi bora ambaye alijiamini.

Akiwa mwanafunzi mdogo kiumri kuliko wengine wote darasani kwake. Akiwa na umri wa miaka 11 alianza kujifunza judo na sambo. Yeye alisema huo “si mchezo tu, bali ni falsafa.”

Wakati huo Putin alikuwa tayari anafikiria kwa uzito kuhusu maisha yake ya baadaye. Sinema aliyoiona wakati mmoja kuhusu ujasusi wa Urusi ilimpa Putin hamu ya kusoma kila riwaya aliyoweza kuipata kuhusu ujasusi.

Hatimaye, aliamua kwamba njia bora zaidi ni kuwasiliana na Idara ya Usalama na Shirika la Ujasusi la Urusi (KGB) moja kwa moja. Alienda kwenye makao makuu ya KGB eneo la Leningrad na kueleza kwamba alitaka kujua jinsi ya kujitolea kwa ajili ya KGB.

Itaendelea kesho