Maiti yasafirishwa kwenye kiroba, familia yachachamaa

Maiti yasafirishwa kwenye kiroba, familia yachachamaa

Muktasari:

  • Ukweli ni upi, hili ndio swali kuu baada ya familia ya kijana Setas Tarimo (36) kudai mwili wake ulisafirishwa ukiwa katika mfuko wa sandarusi maarufu kama `kiroba’, lakini waliomsafirisha wakipinga vikali madai hayo.

Moshi/Rombo. Ukweli ni upi, hili ndio swali kuu baada ya familia ya kijana Setas Tarimo (36) kudai mwili wake ulisafirishwa ukiwa katika mfuko wa sandarusi maarufu kama `kiroba’, lakini waliomsafirisha wakipinga vikali madai hayo.

Mbali na madai hayo, ndugu wanadai mwili wa kijana huyo aliyefariki dunia Aprili 4 mwaka huu, ulisafirishwa kwa usafiri wa basi dogo aina ya Hiace maarufu kama daladala kutoka Mbweni mkoani Pwani hadi kijiji cha Lessoroma kilichopo wilaya ya Rombo.

Hata hivyo, mmoja wa watu waliosafirisha mwili huo kutoka Pwani, Mohamed Omary amepinga madai hayo akisema waliusitiri kwa kuufunga na mashuka meupe masafi na kuufunga kwenye mkeka kama maiti nyingine zinavyosafirishwa kwa heshima.

Mohamed alisema wakati alipoanza kuumwa malaria na baadae ugonjwa kama wa kifafa, walimpigia simu mama yake ambaye aliwaambia hali kama hiyo ilikuwa ikimtokea pia huko Rombo, lakini walikuwa wakimpeleka kwenye maombi.

“Hakufia hospitali bali alifia nyumbani kwa hiyo tukawasiliana na tajiri yake ambaye alituma Sh200,000 za mafuta lakini usafiri tulikubaliana na ndugu mmoja anaitwa Tarimo kuwa tukifika wangelipia hilo gari,” alieleza Mohamed.


Kwa upande wake, Kamanda wa polisi Mkoa wa Klimanjaro, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP), Amon Kakwale alithibitisha suala hilo kupelekwa kituo cha polisi Usseri lakini alieleza lilikuwa suala la madai.

Kwa habari kamili usikose kujipatia gazeti la Mwananchi leo.