Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Majaliwa aeleza mikakati ya Serikali uchumi wa digitali

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiangalia namna ya utoaji wa mafunzo ya teknolojia na masomo ya sayansi kwa wanafunzi wa kike kupitia programu ya ‘Code Like a Girl’ inayoendeshwa na Vodacom Tanzania nchini, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Future Ready Summit uliofanyika jijini Dar es Salaam leo Februari 15 2024. Kulia ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye. Picha na Michael Matemanga


Muktasari:

Imeelezwa kuwa, azma ya Serikali ni kuwekeza katika huduma zote, ili ziwe za kidijitali na kuzuia watu kukutana na kuondoa kushawishiana kuombana rushwa

Dar es Salaam. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali inaendelea kuwekeza nguvu katika ulimwengu wa teknolojia, ili kuwa na uchumi wa kidijitali kama mwelekeo wa dunia ulivyo sasa.

Majaliwa amesema moja ya faida ya kuwekeza kwenye dijitali ni kuondokana na rushwa, ubadhirifu na hata wizi.

Akizungumza kwenye kongamano la kiteknolojia la 'Future Ready Summit' lililoandaliwa na Kampuni ya Vodacom, Majaliwa leo Alhamisi Februari 15 2024 amesema lazima kuwepo ushirikiano kati ya sekta binafsi na Serikali, ili kufikia malengo hayo.

“Teknolojia inazuia watu kukutana kwa kuwa shughuli zote zinamalizika mtandaoni, hivyo hili linaepusha rushwa, wizi, ubadhirifu. Mfano kwa sasa watu wanalipa ada, nauli hata kufanya maombi kidijitali, hawakutani," amesema.

Pia, amesema azma ya Serikali ni kuwekeza katika huduma zote, ili ziwe za kidijitali na kuzuia watu kukutana na kuondoa kushawishiana kuombana rushwa.

“Jambo hilo pia, linapunguza gharama za uendeshaji, linarahisisha huduma, linaokoa muda na kurahisisha mawasiliano, ikiwamo ya kibiashara, hivyo itachochea ukuaji wa uchumi wa kidijitali," amesema Majaliwa.

Katika hilo, amesema fursa za kidijitali zinaongezeka duniani na Serikali inaendelea kuimarisha ukuaji wa matumizi hayo ili kufikia malengo ya kujenga Tanzania ya kidijitali.

Amesema jambo kubwa ni kuwekeza katika miundombinu kwa kushirikiana na kampuni binafsi na ndiyo maana Serikali inaendelea kujenga minara na  mpaka sasa imeshajengwa 292 kote nchini kati ya 758, lengo likiwa kila Mtanzania apate huduma ya mawasiliano ya kiteknolojia, ikiwamo intaneti.

Pia, amehimiza mitandao ya simu kuweka gharama nafuu.

Awali, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema mambo yote yanatokana na sera nzuri zinazoongoza wizara.

“Sera zinahakikisha uwekezaji kwenye miundombinu, vyuo, taasisi, ujenzi wa minara. Tanzania iko tayari kwenda mbele na mapinduzi haya. Tunataka huduma zipatikane kwa ubora, hakika, salama na zenye matokeo kwa watu wetu,” amesema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Vodacom, Philip Besiimire amesema katika kufanikisha ukuaji wa huduma ya kidijitali, Vodacom imeamua kukopesha simu ili kuhakikisha kila Mtanzania anamiliki.

Mkuu wa Idara ya Kitovu cha Akili Bandia kutoka ITU, Sofie Maddens amesema kinachohitajika ni muunganiko na mshikamano kwa jumla.

Maddens  amesema kuna vijana wengi wanahamu ya kunifunza teknolojia, hivyo nguvu inahitajika na hata sekta binafsi zinapaswa kuwekeza zaidi.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), Dk Mwinuka Lutengano amesema matumizi sahihi ya teknolojia hasa Tehama yana msaada mkubwa na hata kuwa na fursa ya kuongeza ufanisi kwenye shughuli nyingi.