Majaliwa mgeni rasmi swala ya Eid El-Adha

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Muktasari:

  • Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika swala ya Eid El- Adha ambayo inatarajiwa kuwa Alhamisi Juni 29 mwaka huu.

Dar es Salaam. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika swala ya Eid El- Adha ambayo inatarajiwa kuwa Alhamisi  Juni 29 mwaka huu.

Hayo yameelezwa leo Juni 22 na  Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir katika hafla fupi ya kumbukizi ya miaka 8 ya uongozi wake.

Amesema swala hiyo kitaifa itafanyika jijini Dar es Salaam katika Msikiti wa Mfalme Mohamed VI Bakwata Makao Makuu Kinondoni kuanzia saa 1.30 asubuhi na kufuatiwa na Baraza la Eid baada ya swala katika msikiti huohuo.

"Ninawasihi waumini watakaohudhuria ibada hiyo katika msikiti Msikiti wa Mfalme Mohamed VI kubaki baada ya swala ili waweze kuhudhuria Baraza la Eid na pia anawatakia Waislamu na wananchi wote maandalizi mema ya Sikukuu hiyo," amesema.