Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Majeruhi 15 wapokewa Dodoma, wengi waumia kichwani na mikononi

Muktasari:

  • Majeruhi waliofikishwa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma wako 15, wanaume 12 na wanawake watatu, wengi wameumia kichwani na mikononi.

Dodoma. Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma, Dk Ernest Ibenzi amethibitisha kupokea majeruhi 15 wa ajali hiyo.

Hayo yamesemwa leo Alhamisi Februari 9, 2023 na Dk Ibenzi alipopigiwa simu kuhusu majeruhi hao wa ajali ya basi la abiria na lori yaliyogongana uso kwa uso usiku wa kuamkia leo katika Kijiji cha Sirwa, Kata ya Pandambili wilayani Kongwa na kuababisha vifo 12 huku majeruhi wakiwa 63.

Dk Ibenzi amesema 12 ni wanaume na watatu ni wanawake ambapo amedai wengi wameumia kichwani na mikononi.

Amesema wanaendelea kuwapatia matibabu na wale watakaopata nafuu watawaruhusu kurudi nyumbani.


Kauli ya DC Kongwa
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa mkoani hapa, Remidius Mwema amesema majeruhi wa wako 63, wanaume 40 wanawake 23.

Ajali hiyo imehusisha basi la Frester lililokuwa likitokea Bukoba mkoani Kagera kwenda Dar es Salaam baada ya kugongana na lori uso kwa uso katika Kijiji cha Sirwa usiku wa kuamkia leo.

Amesema majeruhi 36 wapo katika Hospitali ya Wilaya ya Gairo, majeruhi 27 walipelekwa katika kituo cha Afya cha Kibaigwa ambapo kati ya hao 16 walihamishiwa Hospitali ya Wilaya ya Kongwa kwa matibabu zaidi na wengine walipelekwa Dodoma kutokana na hali zao kuwa siyo nzuri.

Tutaendelea kuwaletea taarifa zaidi ya ajali hii. Endelea kufuatilia tovuti hii na mitandao yetu ya kijamii.