Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Majina ya wanaorejea soko la Kariakoo haya hapa

Muktasari:

  • Soko la Kariakoo limekarabatiwa na kuongezwa maeneo mapya baada ya kuungua Julai 10, 2021 na kuteketeza mali za wafanyabiashara.

Dar es Salaam. Hatimaye majina 1,520 ya wafanyabiashara walio na sifa na vigezo vya kurejea katika Soko Kuu la Kariakoo yamewekwa hadharani.

Sanjari na hilo, wafanyabiashara zaidi ya 366, hawataruhusiwa kurudi sokoni hapo hadi watakapolipa madeni waliokuwa wanadaiwa na Shirika la Masoko kabla soko halijaungua.

Hatua hii inakuja baada ya kukamilika kwa ukarabati na ujenzi wa ghorofa ulioanza baada ya soko kuungua Julai 10, 2021, ambapo na serikali ilitoa Sh29 bilioni ili lifanyiwe ukarabati ambao ulienda sanjari na ujenzi mpya wa soko dogo.

Jana Ijumaa Januari 31, 2025 taarifa kwa vyombo vya habari, iliyotolewa na Ofisa Uhusiano Mkuu wa shirika hilo, Revocutus Kasimba, ilisema orodha ya  majina hayo ya watakaorejeshwa yatapatikana kwenye tovuti ya <https://www.kariakoomarket.co.tz/> na iIe ya Ofisi ya Rais-Tamisemi  <https://www.tamisemi.go.tz/>

Hata hivyo, Kasimba amesisitiza wale wafanyabiashara 366 wanaodaiwa na Shirika zaidi ya Sh358 watapaswa kulipa deni hilo kabla hawajapatiwa nafasi za biashara.

Kabla ya hatua hii, mchakato wa kutoa majina ya waliopitishwa kurejea kwenye uhakiki ulikwama Julai 2024 baada ya orodha ya awali kugomewa na wafanyabiashara kwa kile walichodai viongozi wao hawakushirikishwa.

Hata hivyo, ili kufikisha kilio chao hicho Julai 12, 2024 walikusanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja kisha kuandamana hadi ofisi ndogo za Chama cha Mapinduzi, Lumumba jijini hapa.

Julai 13,2024 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, alikutana nao na kuridhika na hoja zao, ambapo pamoja na mambo mengine  aliamuru majina 819 yaliyokuwa yamepitishwa yaondolewe kwenye mfumo na kufanyika uhakiki upya.

Januari 30, 2025 Mwenyekiti wa Bodi ya shirika hilo, Hawa Ghasia, aliwaeleza waandishi wa habari kuwa uhakiki huo umeshakamilika na orodha mpya ingetolewa wiki hii.