Makalla atoa elimu ya kuhamisha wamachinga kwenye maeneo rasmi

Makalla atoa elimu ya kuhamisha wamachinga kwenye maeneo rasmi

Muktasari:

  • RC Makalla ametumia ziara yake ya jimbo kwa jimbo mkoani humo kutoa elimu kwa wamachinga kuhamia maeneo yaliyo rasmi.

Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla ametumia ziara yake ya jimbo kwa jimbo mkoani humo kutoa elimu kwa wamachinga waofanya biashara zao katika maeneo yasiyo rasmi na kuhamia maeneo yaliyo rasmi.

Makalla namefanya hivyo leo Jumatano Septemba 22, 2021 ikiwa imepita siku tano tangu mkoa huo uzindue mwongozo wa kuwapanga wafanyabiashara hao.

Katika ziara ya leo ambapo alikwenda Kata ya Mabwepande wilaya ya Kinondoni, alisimaamisha msafara wake kituo cha daladala Bunju na kutoa elimu kwa wafanyabiashara hao kuhusu umuhimu wa kuwahamisha maeneo hayo.

Pia alifanya hivyo wakati alipomaliza mkutano wake katika kituo cha daladala Tangi Bovu Mbezi Beach.

Akiwa hapo alikwenda moja kwa moja kwenye kibanda cha mama lishe na kuanza kumuelimisha akimwambiakuwa anachokifanya cha kuweka kibanda katika eneo la juu ya mtaro ni kitendo kisichokubalika, kwani hata usafi katika mitaro utashindikana kufanyika.

Pia aliwasihi wafanyabiashara waliokuwepo eneo hilo, kutoa ushirikiano siku ya kuwahaisha itakapofika na kueleza kila mtu atapata eneo kwa kuwa Mkoa una maeneo ya kutosha.

Wamachinga wa Jiji la Dar es Salaam, wamepewa mwezi mmoja kukaa katika maeneo hayo kabla ya kampeni ya kuwapanga katika maeneo mbalimbalu rasmi waliyotengewa kuanza