Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Makamba ataja turufu tano za kunufaika na soko la gesi

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

Waziri wa Nishati, January Makamba ametaja sifa tano zinazochagiza mazingira mazuri ya soko la rasilimali ya gesi asilia ikiwamo upekee wa gesi ya Tanzania iliyo na mchanganyiko wa hewa ya kaboni na salfa ndogo zaidi, tofauti na gesi zinazozalishwa mataifa mengine duniani.

Dar es Salaam. Waziri wa Nishati, January Makamba ametaja sifa tano zinazochagiza mazingira mazuri ya soko la rasilimali ya gesi asilia ikiwamo upekee wa gesi ya Tanzania iliyo na mchanganyiko wa hewa ya kaboni na salfa ndogo zaidi, tofauti na gesi zinazozalishwa mataifa mengine duniani.

Makamba ametoa kauli hiyo leo Juni 11, 2022 mjini Dodoma wakati wa kutia saini makubaliano ya awali katika Mkataba Hodhi (HGA), kati ya Serikali na Kampuni za Shell na Equinor ikiwa ni matumaini mapya ya mwelekeo wa utekelezaji wa Mradi wa Kuchakata na Kusindika Gesi Asilia (LNG), Lindi na Mtwara.

“Gesi hii inapendwa na inakimbiliwa dunia, jambo la pili linalofanya upepo uwe upande wetu ni majadiliano ya jumla kuhusu mabadiliko ya tabianchi duniani kuondokana na matumizi ya nishati chafu kwenda safi na gesi asilia siyo safi sana lakini siyo chafu,”amesema Makamba.

Tatu ni fursa ya mwenendo wa Kijiopolitiki duniani unaohusisha watumiaji wakubwa wa nidhati kutafuta vyanzo vipya vya nishati huku Tanzania ikiwa miongoni mwa vyanzo vya uhakika vinavyotazamwa. Nne, Tanzania inanufaika kijiografia kutokana na ukaribu wake katika asilimia 70 ya masoko ya gesi barani Asia.

“Mwisho ni mazingira mapya, imani mpya inayotokana na uongozi wako (Rais Samia Suluhu Hassan), katika kuweka mazingira bora ya uwekezaji hatua iliyowafanya wenzetu (wawekezaji) warudi,”amesema.