Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Makandarasi wa ndani kicheko

Muktasari:

  • Serikali imesema haipendi kuona makandarasi wa ndani wakiendelea kuidani wakati wameshafanya kazi, hivyo imetenga fedha kuanzia Agosti 2023, kwa lengo la kulipa madeni hayo na inatarajia kuyamaliza ifikapo mwezi ujao.

Mwanza.  Serikali imesema imejidhatiti  kuhakikisha inalipa madeni yote ya makandarasi wa ndani hadi ifikapo Novemba, mwaka huu, baada ya kupatiwa maelekezo na Rais Samia Suluhu Hassan.

Itakumbukwa, katika moja ya maagizo yake kwa Wizara ya ujenzi, Rais Samia alisema anataka kuona wizara hiyo inamaliza kadhia hiyo ya madeni na alitoa maelekezo kwa waziri mwenye dhamana kutekeleza hilo.

Akizungumza leo jijini Mwanza katika mkutano wa makandarasi ulioambatana na mafunzo ya kozi maalumu ya usimamizi wa mikataba ulioandaliwa na Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB), Waziri wa Ujenzi, Innocent  Bashungwa alisema tayari walishaanza kutekeleza hilo na Agosti, mwaka huu.

Makandarasi wanaopatiwa mafunzo hayo wanatoka mikoa ya kanda ya ziwa ya Mwanza, Geita, Kagera, Simiyu, Shinyanga na Mara.

Bashungwa amesema, “Serikali haipendezwi na hali hiyo na inajitahidi kuitatua kwa mfano, Mheshimiwa Rais, ameagiza madeni yote ya nyuma ya makandarasi yalipwe. Tumeshaanza utekelezaji tangu Agosti 2023, Serikali imekuwa ikitenga Sh70 bilioni kwa lengo la kulipa madeni hayo ya makandarasi.

Katika hizo, Sh50 bilioni zinalipwa kwa makandarasi wa ndani na Sh20 bilioni kwa makandarasi wageni kila mwezi.”

Waziri huyo amesema kupitia mpango huo, hadi kufikia Novemba, madeni yote ya makandarasi yatakuwa yameshalipwa.

Kauli hiyo ya Bashungwa ameitoa baada ya kupokea maombi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB), Mhandisi Joseph Nyamhanga kwa niaba ya makandarasi, kutaka changangoto ya ucheleweshwaji wa malipo yao.
Amesema hali hiyo huchangia kuwakwamisha kwenye ukamilishaji wa miradi kwa wakati.

Nyamhanga amesema; “Mheshimiwa Waziri changamoto hii ni kubwa na inawaathiri sana makandarasi wa ndani na hivyo ninaomba uichukue na kuona jinsi ya kuitatua.”

Kwa upande wake, Msajili wa Bodi ya Makandarasi, Mhandisi Rhoben Nkori amesema Bodi hiyo inafanyia kazi maelekezo ya wizara na kutengeneza mpango mkakati wa kuwawezesha makandarasi wa ndani kupata zabuni zinazotolewa na Serikali.

“Mheshimiwa waziri hukupendezwa na uwiano wa kazi zinazotolewa kwa makandarasi wa ndani na wa nje, sisi kama taasisi tumeshaweka mikakati na kilichosalia sasa ni kuandaa ripoti ambayao itawasilishwa mezani kwako,” amesema Nkori.

Mkutano huo pia umelenga kutoa mafunzo kwa makandarasi ya mfumo mpya wa manunuzi kwa njia ya mtandao (NeST).