Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Malipo kwa nja ya simu yaongeza fursa za kujiajili mtandaoni

Vijana na wanawake nchini Tanzania, kama katika mataifa mengine ya Afrika , wanazidi kujiajiri kwa kufanya biashara mtandaoni kupitia zimu za mkononi. Kati ya fursa hizi ni uuzaji wa moja kwa moja ambao nimfumo raihisi wa biashara unaohitaji mtataji mdogo.

 Umaarufu wa biashara za moja kwa moja umezidi kuongezeka hususan Afrika Masharaki kutokana na nchi hizo kuwekeza katika kuboresha miundombinu ya mawasiliano kama vilie upatikanaji wa intaneti na minara ya mawasiliano.

 "Sekta ya uuzaji wa moja kwa moja barani Afrika leo iko katika hatua ya ukuaji na tasnia hii inakua kwa kasi kwa sababu ya kuongezeka kwa wajasiriamali wadogo wadogo," anafafanua bwana Biram Fall, Meneja Mkuu wa QNET Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Katika mawasiliano yake na vyombo vya habari mwishoni  mwa wiki hii, menjeza huyo alitangaza uzinduzi wa malipo ya fedha kwa njia ya simu kwa wawakilishi wao nchini Tanzania, Kenya na maeneo mengine ya Afrika.

“Kwa kweli ni vigumu kupata kampuni inayofanya biashara ya moja kwa moja barani Afrika ambayo haina kipengele cha malipo kwa njia ya simu, hivo na sisi sasa tumezindua malipo kwa njia simu kusaidia kukuza biashara za wa wakilishi wetu,” alielezea.

"Mfumo wa biashara za moja kwa moja unatoa ajiri nyingi maana unahitaji mtaji mdogo tu kuanza, jambo ambalo hurahisisha vijana na wanawake kujiajiri," aliongeza.

Kwa upande mwingine, uuzaji wa moja kwa moja unakua kwa kasi kutokana na kuongezeka kwa biashara ya mtandaoni Afrika.

Katika ripoti ya McKinsey inaonyesha kuwa thamani ya soko la mtandaoni Afrika itafikia zaidi ya dola za kimarekani trilioni 2.1 ifikapo mwaka 2025. Ripoti hiyo pia inasema, kwa sasa, zaidi ya asilimia 40 ya Waafrika wote wanaweza kupata aina fulani ya mtandao jambo ambalo linapelekea kuongezeka kwa huduma za mtandaoni.

"Swala lingine lililo pelekea kuongezeka kwa biashara za mtandaoni ni janga la uviko 19,” alisema bwana Fall. Kipindi cha uviko 19 watu wengi walizuiiwa kusafiri hivo kuanza kufanya biashara mtandaoni badala ya kukutana uso kwa uso.

“Janga hilo lilifanya wasambazaji na wateja kutegemea shughuli za biashara ya kielektroniki ili kukidhi mahitaji yao ya bidhaa," aliendelea kufafanua.

Kufikia 2019, malipo kwa njia ya simu yalikuwa na watumiaji zaidi ya bilioni 1 barani Afrika. Mifumo ya malipo ya simu kama vile M-Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money na zingine inazidi kukua kwa kasi na biashara nyingi zinajikita kupokea malipo kwa njia ya simu.

Kwa kuzingatia maendeleo haya, QNET, moja ya kampuni  kubwa za biashara ya moja kwa moja sasa imezindua malipo kwa njia ya simu, alisema bwana Fall.

Faida kubwa ya kutumia malipo kwa njia ya simu ni urahisi wakuwafikia wateja na kupunguza usumbufu wa kwenda benki au madukani kununua bidhaa.

"Kwa kuanzishwa malipo kwa njia ya simu, QNET inataka kurahisisha ufanyaji wa kazi kwa wasambazaji wake na kuwasaidia kukuza biashara zao," alisema.

Kampuni hio imezindua malipo kwa njia ya simu imezindua nchini Tanzania, Kenya, Rwanda, Uganda, Burundi, na Ghana na inapanga upanuzi zaidi katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Nchini Tanzania, malipo yanapatikana kupitia kampuni zote maarufu za mawasiliano zikiwemo Airtel, Tigo na M-Pesa ya Vodacom. Nchini Kenya ni M-Pesa, Airtel Money na Equitel wakati nchini Uganda malipo yanaweza kufanywa kupitia MTN na Airtel.

Nchi nyingine ni Burundi (Econet), Cameroon (MTN, Orange Money), Ghana (MTN, Airtel Tigo, Vodafone) na nchini Zambia (MTN, Zamtel, Airtel).