Mara yapata Sh197 milioni za ujenzi wa mabweni

Muktasari:

  • Halmashauri ya Wilaya ya Butiama mkoani Mara imepoeka zaidi ya Sh197.8 milioni kutoka mpango wa kunusuru kaya maskini nchini  kwaajili ya kutekeleza ujenzi wa mabweni ya wanafunzi  katika shule ya Sekondari Bumaswa katika halmashauri hiyo.

Butiama. Halmashauri ya Wilaya ya Butiama mkoani Mara imepoeka zaidi ya Sh197.8 milioni kutoka mpango wa kunusuru kaya maskini nchini  kwaajili ya kutekeleza ujenzi wa mabweni ya wanafunzi  katika shule ya Sekondari Bumaswa katika halmashauri hiyo.

Mabweni hayo yanatarajiwa kuwanufaisha wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo kutoka Kata ya Bwiregi ambao baadhi hutembea kilomita 32 kwenda na kurudi shule kila siku.

Akitoa taarifa kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,  Mohammed Mchengerwa aliyefanya ziara katika halmashauri hiyo leo Oktoba 7, 2021, Leopold Costantine amesema ujenzi wa mabweni hayo umeanza mwezi uliopita utakamilika Novemba mwaka huu.

Amesema kuwa lengo la mradi huo wa mabweni ni kuboresha taaluma katika halmashauri hiyo kwa kuondoa vikwazo wanavyokutana navyo wanafunzi ikiwemo suala la kutembea umbali mrefu kwenda shuleni.

Amesema kuwa katika mradi huo jamii inatakiwa kuchangia Sh17.8 milioni kwaajili ya kukamilisha mradi huo na tayari michango imeanza kwa njia mbalimbali ikiwemo nguvu kazi.

Amesema halamshauri hiyo imepokea zaidi ya Sh7.4 milioni kwaajili ya kuwawezesha walengwa wa mpango huo wa kunusuru kaya maskini ambapo kaya 6,335 zenye walengwa 31,675 wamenufaika.

Akizungumza baada ya kupokea taarifa hiyo, Waziri Mchengerwa amesema kuwa mpango wa kunusuru kaya masikini pia unaolenga kuboresha miundombinu ya huduma za kijamii ili jamii ipate huduma bora.

Mchengerwa amesema ameridhishwa na utekelezaji wa mpango huo mkoani Mara ambapo amewataka waratibu wa mpango huo nchini kujifunza kutoka kwa waratibu wa Mara.

" Hapa mpango umetekelezwa vizuri sana tofauti na mikoa mingine ambapo tumekuta kuna upungufu mkubwa, naomba niwaagize muhakikishe kuwa kila Mtanzania mwenye sifa za kuwa mnufaika wa huu mpango  anajumuishwa na hakuna kumuacha nyuma maana nimepewa fedha nyingi sana na Rais na ni lazima zitumike na kuleta matokeo chanya" amesema

Mwisho

Summary

Mpango wa kunusuru kaya masikini nchini umetoa zaidi ya Sh197.8 milioni kwaajili ya ujenzi wa mabweni mawili katika shule ya Sekondari Bumaswa wilayani Butiama.

Mara yapata Sh197 milioni za ujenzi wa mabweni

Beldina Nyakeke, Mwananchi [email protected]