Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mashiba: Vijana wafundishwe kutumia mabando kujipatia fedha

Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote UCSAF, Justina Mashiba

Muktasari:

  • Wakati vilio vya bando vikiwa bado vinasikika sehemu tofauti, Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote amependekeza watu watumie intaneti kujitengenezea fedha.

Dar es Salaam. Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Justina Mashiba amesema umefika wakati wa vijana kufundishwa namna ya kutumia mabando yao kujipatia fedha badala ya shughuli zisizokuwa na maana.

Hiyo ni kutokana na kile alichoeleza kuwa licha ya kuwapo kwa kelele juu ya bando lakini baadi wamekuwa wakizifanyia kazi zisizokuwa na faida

Ameyasema hayo katika Mwananchi Jukwaa la Fikra lililoandaliwa na Mwananchi Communications Limited likijadili mada isemayo “Mabadiliki ya kidigitali kwa ajili ya ustawi na ushirikishwaji wa jamii Dira 2025”.

Akizungumza katika kongamano hilo, Justina amesema takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 63 ya Watanzania wanapata huduma ya intaneti lakini endapo utafiti ukifanyika wengi hawawezi kuwa wanatumia kwa manufaa.

"Unaweza kukuta watu wanaingia Instagram wanachapisha picha ambazo wakati mwingine haziwapi hata fedha nafikiri ni wakati sasa wa kuangalia nini tunatumia katika intaneti, wakati mwingine tunalalamika gharama za bando ni kwa sababu hatutumii bando kwa manufaa," amesema Justina.

Amesema ni vyema kufika wakati ambao watu watatumia bando kwa manufaa.

"Kuna msichana mdogo ambaye amekuwa akitengeneza  Sh2 milioni kwa mwezi kupitia ya mitandao ya kijamii unapotumia vizuri unaweza kupata fedha nyingi tunatakiwa kuhamasisha wengi wajue hili," amesema Justina.

Amesema Serikali inatambua kuwa haiwezi kuzungumzia huduma za kifedha jumuishi bila huduma za mawasiliano ndiyo maana nguvu kubwa imekuwa ikitumika katika kuhamisha matumizi ya mtandao.

Alisema anaamini kuwa siku moja gharama hizo zitashuka na tozo kuondolewa baada ya watu wengi kuingia katika matumizi ya simu za mkono au kuunganishwa na mawasiliano.

"Kwa sasa uwekezaji ni gharama, tunaenda mpaka vijijini kufikisha huduma za mawasiliano nafikiri tukimaliza kila kitu kitabadilika.