Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Matinyi awatoa hofu waandishi waliozuiwa kutekeleza majukumu yao

Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi.

Dar es Salaam. Serikali imesema vyombo ya habari binafsi na waandishi wa habari wa kujitegemea wataendelea kutekeleza majukumu yao kwa uhuru na kutoa ushirikiano kwa Serikali.

Hayo yameelezwa kufuatia katazo batili la Halmashauri ya Mji wa Ifakara mkoani Morogoro la kuwataka waandishi na vyombo vyao kutochukua na kuandika taarifa za Serikali “bila idhini au mwongozo wa Serikali.”

Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi amesema katazo hilo si sahihi na tafsiri ya sheria na Katiba iliyotolewa kuhalalisha katazo hilo ni potofu.

Tamko la Matinyi limetokana na taarifa iliyotolewa kwa umma Oktoba 9, 2023 na Kaimu Mkuu wa Mawasiliano serikalini katika Halmashauri ya Mji wa Ifakara, ikitaka kuaminisha umma kuwa “jukumu la kutoa habari za Serikali na matangazo ya Serikali ni la chombo cha habari cha Serikali au ofisa habari wa Serikali.

Kulingana na taarifa hiyo, yeyote atakayetenda kinyume na utaratibu huo angekuwa anafanya kosa kisheria kwa mujibu wa kifungu cha 7 kifungu kidogo cha 1 (b) (iv) cha Sheria ya Huduma Habari ya mwaka 2016.

"Chombo binafsi cha habari au mwandishi binafsi wa habari hakitakiwi kutoa habari au kuzungumzia masuala mbalimbaili ya Serikali bila idhini au mwongozo wa Serikali,” ilinukuliwa taarifa hiyo, iliyosambaa kwenye vyombo vya habari.

Pia, kwenye taarifa hiyo ilinukuu Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 18 (1), ambayo inatoa haki ya uhuru wa mawazo kwa Mtanzania yeyote yule.

Akinukuu ibara hiyo, alisema Katiba inaruhusu, “Kutoa nje mawazo yake, kutafuta, kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi na pia na uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa, lakini bila kuathiri sheria za nchi,” ilisema taarifa hiyo.

Baada ya tamko hilo lililozua mjadala na sintofahamu mitandaoni, Msemaji Mkuu wa Serikali alitoa taarifa kwa umma akisema tafsiri ya kisheria iliyotolewa kuhusu suala hilo si sahihi.

Matinyi alisema, “Sheria ya Huduma za Habari sura ya 229 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2023, haijakataza wala kuzuia vyombo vya habari vya kujitegemea na waandishi wa habari wa kujitegemea kutoa tarifa za Serikali, isipokuwa kwa taarifa ambazo zimezuiliwa kwa mujibu wa Sheria.

“Kifungu cha 7 (1), Sheria imeweka bayana haki za msingi za vyombo vya habari na waandishi wa habari ambazo ni kutafuta, kuchakata na kutangaza au kuchapisha habari,” alisema kupitia taarifa hiyo.

Alisema kifungu cha 7(2) (b) (iv) kinaeleza wajibu wa vyombo vya habari binafsi katika kutangaza masuala yenye umuhimu kwa Taifa na si katazo wala kosa kwa vyombo hivyo kutoa taarifa, habari na matangazo ya Serikali.

Hivyo, Matinyi (pichani kulia) alitoa wito kwa vyombo ya habari na waandishi wa habari kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa uhuru na kutoa ushirikiano kwa Serikali, hasa katika kutangaza miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya sita.

Lakini pia amevielekeza vyombo vya habari kuzingatia sheria, kanuni, weledi na maadili ya uandishi wa habari.