Matokeo kidato cha nne 2022 haya hapa
Muktasari:
Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya mitihani ya kidato cha nne yaliyofanyika Novemba 14 hadi Desemba 1, 2022, Tanzania Bara na Visiwani.
Dar es Salaam. Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya mitihani ya kidato cha nne yaliyofanyika Novemba 14 hadi Desemba 1, 2022, Tanzania Bara na Visiwani.
Matokeo hayo yametangazwa leo Jumapili, Januari 29, 2023, makao makuu ya Necta jijini Dar es Salaam na Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Athumani Amasi.