Matumizi ya EFD yafunga maduka 30
Muktasari:
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imefunga maduka 30 ya vituo cha mafuta na mgahawa kwa kutotumia mashine za kodi za kielektroniki (EFD).
Arusha. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imefunga maduka 30 ya vituo cha mafuta na mgahawa kwa kutotumia mashine za kodi za kielektroniki (EFD).
Maofisa wa TRA waliendesha operesheni katika mitaa mbalimbali Arusha na kufunga maduka hayo.
Meneja msaidizi wa TRA Mkoa wa Arusha, Alex Katundu alisema wamefanya operesheni hiyo baada ya kuwabaini baadhi ya wafanyabiashara hawazitumii mashine hizo.