Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbaroni akidaiwa kuwatukana viongozi wa Serikali

Muktasari:

  • Mkazi wa Kigamboni, Selemani Gaya (18) amekamatwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa tuhuma za kutoa lugha ya matusi mtandaoni dhidi ya viongozi wakuu wa Serikali ya Tanzania.

Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linamshikilia Selemani Gaya (18) mkazi wa Kigamboni, kwa tuhuma za kutoa lugha ya matusi mtandaoni dhidi ya viongozi wakuu wa Serikali ya Tanzania.

 Ripoti iliyotolewa na jeshi hilo imesema, mtuhumiwa huyo aliyekamatwa Julai 29, 2023 amekuwa akishirikiana na wenzake kutengeneza maudhui ya mtandaoni kuwatukana na kuwafedhehesha viongozi wa Serikali na kusambaza kwenye kurasa zao za Tiktok.

“Mtuhumiwa huyu atafikishwa mahakamani haraka izekanavyo,” imesema raarifa hiyo.

“Jeshi la Polisi linatoa onyo kali kwa mtu anayetoa toa lugha za matusi na fedheha kwa Viongozi wa Serikali kwa njia ya mtandao na njia nyingine yoyote,” imeongeza taarifa hiyo.

Aidha imesema kuwa Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na mamlaka nyingine za kisheria limejipanga kuwafuatilia na kuwakamata, kuwahoji kwa kina wahalifu hao na hatimaye kuwafikisha haraka kwenye vyombo vya sheria.