Mbowe atoa msimamo wa Chadema TCD

Muktasari:

  • Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ametoa msimamo wa chama hicho wa kutoshiriki mkutano wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) na kongamano linalotarajiwa kufanyika Machi 30 na 31, 2022 jijini Dodoma.


Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ametoa msimamo wa chama hicho wa kutoshiriki mkutano wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) na kongamano linalotarajiwa kufanyika Machi 30 na 31, 2022 jijini Dodoma.

Ameyasema hayo leo Machi 18 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za makao makao makuu ya chama hicho jijini hapa.

“Tarehe 21 (Machi 21) nimeambiwa kuna kikao cha TCD, Chadema tulikubaliana hatutashiriki kwa kuwa hatuna wabunge hadi hali hii itakapobadililllka.

Amezungumzia pia kongamano la TCD linalotarajiwa kufanyika Machi 30 na 31, 2022 kwa lengo la kutafuta maridhiano ya kisiasa akisema hawatashiriki.

“Hatutashiriki kongamano la TCD na hao wanaosema nimeridhia kushiriki kongamano wapi nimeridhia?

“Hatuoni mkakati wa kutupata Katiba mpya ipo agenda ya kuahirisha suala la katiba mpya sio Mbowe wala kiongozi yoyote wa Chadema atakayeshiriki,” amesema.

Mbowe: Chadema haijawahi kuteua wabunge 19

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kuwa Spika wa Bunge ameshaandikiwa barua na anajua wabunge 19 wa viti maalumu sio wabunge walioteuliwa na chama hicho. Soma zaidi