Mbunge ahoji kukatika kwa umeme Benjamini Mkapa

Mbunge wa Arumeru Magharibi, Noah Saputu akiomba mwongozo wa kutaka kujua ni kwa nini uwanja wa Benjamini Mkapa unalitia aibu Taifa kwa kukatika umeme leo Bungeni jijini Dodoma.Picha na Merciful Munuo

Muktasari:

  • Sakata la kuzima kwa taa za Uwanja wa Benjamini Mkapa katika mchezo kati ya Yanga na Rivers ya Nigeria leo limetua bungeni, mbunge akisema ni aibu kwa taifa.

Dodoma. Sakata la kuzima kwa taa za Uwanja wa Benjamini Mkapa katika mchezo kati ya Yanga na Rivers ya Nigeria leo limetua bungeni, mbunge akisema ni aibu kwa Taifa.

Hata hivyo Naibu Spika wa Bunge Mussa Zungu amesema kuwa jambo hilo halitajitokeza tena kwani wahusika wametafuta wataalamu wa kufanya ukarabati wa uwnaja mzima na tenda yake inafunguliwa leo.

Awali baada ya kipindi cha maswali na majibu bungeni,Mbunge wa Arumeru Magharibi Noah Saputu aliomba mwongozo wa kutoaka kujua ni kwa nini uwnaja wa Benjamini Mkapa unalitia aibu Taifa kwa kukatika umeme.

“Hivi Karibuni umeme katika uwanja huo ulizima wakati timu ya Taifa ilipokuwa ikicheza na Timu ya Taifa ya Uganda, juzi tena ulizimama wakati timu ya Yanga ikicheza na Rivers, hii ni aibu kwa taifa,” alihoji Saputu.

Naibu Spika alikiri ukweli kuwa Taifa linapata aibu kutokana na yanayotokea katika uwanja huo, lakini akasema Serikali imeshachukua hatua mbalimbali kukabiliana na mapungufu hayo.

Amesema leo tenda ya mtu anayekwenda kufanya ukaguzi na ukarabati wa uwanja mzima ikiwemo masuala ya taa ambao alisema utasaidia kujua chanzo kilikuwa nini lakini akataka Watanzania kutokuwa na mashaka kwani tatizo halitajirudia.