Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbunge ataka kampuni za simu zifidie wateja

Mbunge wa Ulyankulu (CCM), Rehema Migilla akiuliza swali bungeni leo Jumatatu Februari 6, 2022. Picha na Said Khamis

Muktasari:

  • Malalamiko ya kasi ndogo ya mitandao na simu katika baadhi ya maeneo limemuibua Mbunge wa Ulyankulu, Rehema Migilla akitaka fidia kwa wateja wanaokumbana na changamoto ya kasi ndogo ya huduma.

Dodoma. Mbunge wa Ulyankulu (CCM), Rehema Migilla ametaka kampuni za simu katika jimbo lake ambayo yamekuwa yakitoa huduma zenye kasi ndogo kuwafidia wananchi.

Akiuliza swali leo Jumatatu Februari 6, 2022 wakati akiuliza swali la nyongeza amesema huduma za simu na minara ya simu ni biashara na mwananchi anapotoa fedha zake kwa ajili ya kukunua vocha na mtandao anahitaji huduma nzuri.

Amesema, lakini cha ajabu kutokana na kasi ndogo ya minara katika eneo hilo huduma za simu mwananchi zinafikia muda wake kuisha ili hali ikiwa hajapata huduma aliyoikusudia.

“Je, hizi kampuni za simu ziko tayari kuwafidia hawa wananchi wetu ambao fedha zao zimetumika bila kupata huduma kwa sababu huu ni wizi kama wizi mwingine,”amehoji Rehema.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Methew Kundo amesema minara iliyopo katika maeneo hayo katika kata ya Nhwande inauwezo wa 2G pekee yake haijaanza kutoa huduma ya 3G.

Amesema mpango ni kuiboresha kufikia 3G hadi 4G na kwamba wakifikia katika kiwango hicho huduma itaweza kutolewa bila shida yoyote.