Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbuzi, kondoo wazua kizaazaa Moshi

Muktasari:

  • Mbuzi na kondoo wanaozagaa manispaa ya Moshi Mkoa wa Kilimanjaro wametajwa kuwa kero kwa kuharibu miundombinu ya reli na mazingira ya stesheni ya treni.

Moshi. Mbuzi na kondoo wanaozagaa manispaa ya Moshi Mkoa wa Kilimanjaro wametajwa kuwa kero kwa kuharibu miundombinu ya reli na mazingira ya stesheni ya treni.

Hayo yameelezwa jana Ijumaa Mei 28 ,2021 na mkuu wa kituo cha Shirika la Reli (TRC) mjini Moshi, Jaison James wakati wakieleza kero mbalimbali kwa mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk Stephen Kagaigai aliyekutana na taasisi mbalimbali za Serikali.

Ameziomba mamlaka husika kuchukua hatua za haraka na kuwekwa sheria ndogo itakayosaidia kukomesha uzururaji ovyo wa wanyama hao kwenye manispaa hiyo.

"Kuna baadhi ya maeneo mbuzi na kondoo huzagaa sana na huwa kero kubwa hususani maeneo ya stesheni ya reli, wakati mwingine uharibu miundombinu ya reli na mazingira ya stesheni.”

"Tunaziomba mamlaka husika angalau waweke sheria ndogo ambazo zitawezesha kukomesha kero kama hizi za mifugo kwa sababu moshi kihistoria ni mji ambao unasifika kwa usafi, huu uzururaji wa mifugo ovyo unaweza kuweka doa kubwa kwa wageni watakaoingia Moshi," amesema James.

Kwa upande wake Dk Kagaigai amesema  ni kosa kuachia mifugo kuzunguka ndani ya manispaa hiyo kwa sababu wanaharibu mazingira.

"Wale wenye mbuzi na kondoo wanaozurura ovyo ni kosa la kisheria hasa kuingilia miundombinu ya reli na kuharibu mazingira hii ni hatari kubwa mamlaka husika naomba zifanye kazi yake kudhibiti hili wimbi la mifugo kwenye reli maana wanaweza kuleta matatizo makubwa," amesema Rc Kagaigai.